Usajili wa wapigakura huhusisha wadau wengi. Wale wa moja kwa ni raia na asasi za serikali za kusimamia uchaguzi. Lakini wengine huwa na nia ya kujua matokeo ya mchakato wa usajili wa wapigakura kwa kuwa unaweza kuathiri matokeo ya uchaguzi. Wadau hawa ni pamoja na serikali, jeshi, vyama vya kisiasa, makundi yenye nia mbalimbali, asasi za kijamii na za kidini, serikali za mataifa ya kigeni, na mashirika ya kimataifa.
Vyama vya Kisiasa na Usajili wa Wapigakura
Vyama vya kisiasa vina haja kubwa katika shughuli ya usajili wa wapigakura kwa sababu mfumo huo unaotumika unaweza kuathiri moja kwa moja kiwango cha usaidizi vitakaopewa. Mkakati mmoja unaojulikana wa kushinda uchaguzi huwa kudhibiti watu wanaojitokeza kwenye vituo vya kupigia kura: kwa kuchochea au kutatiza usajili wa wapigakura au makundi ya wapigakura, chama kinaweza kuzidisha nafasi zake. Vigezo vitatu vikuu vya utendakazi vya kuhakikisha orodha za wapigakura ni za kisasa, linganifu na kamilifu. Wakati mwingine halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kuwa na ugumu katika kuafiki malengo yake ya utendakazi kwa sababu vyama vya kisiasa vinaweza kuona kwamba kupunguza idadi ya wapigakura au kutenga makundi mengine ya wapigakura kunawapendelea – kwa mfano, watu kutoka maeneo fulani, au makabila fulani. Ikiwa chama kinachojaribu kushawishi usajili wa wapigakura ni chama kilicho mamlakani wakati huo, changamoto hiyo inakuwa kubwa zaidi kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi. Bila shaka si vyama vyote ambavyo hutaka kushawishi hali ya orodha ya wapigakura, lakini wasimamizi wa uchaguzi wanapaswa kutambua uwezekano kwamba vingine vitafanya hivyo.
Vyama vya kisiasa huwa na nia fulani maalumu katika mchakato wa usajili wa wapigakura, na halmashauri za kusimamia uchaguzi pia huwa na nia katika vyama vya kisiasa kwa sababu zifuatazo:
- Vyama vya kisiasa kwa kawaida hutumia orodha ya wapigakura (mara nyingi orodha ya kwanza) kwa minajili ya kampeni. Orodha hiyo huvisaidia vyama kuwasiliana na wapigakura kutoka nyumba moja hadi nyingine kwa njia ya kampeni au kutumia barua.
- Matumizi ya pesa ya chama wakati hutegemea idadi ya wapigakura walio kwenye orodha ya wapigakura. Idadi hii inaweza kutumiwa kudhibiti idadi ya pesa ambazo chama hicho au mgombea wa eneo hilo anaweza kutumia katika kampeni. Idadi ya wapigakura iliyo kwenye orodha hivyo basi inaweza kuwa na athari ya moja kwa moja kwa aina ya kampeni ambayo chama au mgombea anaweza kufanya.
- Ikiwa halmashauri za kusimamia uchaguzi zinafanya usajili wa kutoka nyumba hadi nyingine, na nyongeza ya shughuli wakati wa usajili wa wapigakura, mara nyingi hutegemea vyama vya kisiasa kutoa majina ya watu wanaoweza kufanya kazi kama wasajili. Kwa kuwa usajili wa wapigakura unapaswa kuwa, na kuonekana kama usioegemea upande wowote, wasajili walio na mahusiano na vyama fulani vya kisiasa hufanya kazi wawili wawili, huku kila mmoja wao akiteuliwa kutoka katika chama tofauti.
- Vyama mara nyingi hutekeleza wajibu muhimu, ama kisiri au wazi, kwa kuidhinisha mchakato wa usajili wa wapigakura. Kwa kufanya hivyo, huwa vinakubali uhalali wa uchaguzi huo wenyewe. Kwa manufaa ya uhalali huo, ni muhimu kwamba vyama vya kisiasa vipewe jukumu la kutosha la kuangalia usajili wa wapigakura, na kwamba usajili huo unafanywa bila mapendeleo na kwa njia ya wazi.
Haja za Mataifa ya Kigeni
Serikali za kigeni, mashirika yasiyo ya kiserikali ya kigeni na mashirika mengine ya kimataifa hutoa mchango mkubwa kwa kusaidia katika usimamizi wa uchaguzi wa kidemokrasia, na kwa kutoa waangalizi na huduma za uangalizi wa kimataifa katika uchaguzi. Idhinisho lao linaweza kusaidia pakubwa katika kuhakikisha kwamba uchaguzi unatazamwa kama ulio halali na unaoashiria nia na usemi wa watu.
Haja za Wenyeji
Wadau wa nchini humo kando na vyama vya kisiasa wanaweza kuhisi kwamba wana haja kubwa kushinda waangalizi wa kimataifa katika mchakato wa uchaguzi na matokeo yake, haja hizo ni haki yao. Suala kubwa kwao huwa kutaka kudhibiti serikali. Wadau wengine wanaweza kujaribu kuhusika moja kwa moja katika kampeni badala ya kutoa uangalizi na kusaidia kulweka uhalali katika mchakato huo.
Ikiwezekana, ni bora kuhimiza wadau wote wa nchini kujitahidi kuona kwamba kunakuwa na vyombo na desturi za kuhakikisha kwamba usimamizi wa uchaguzi unakuwa waki na usioegemea upande wowote. Jumuia ya kimataifa inaweza kupendekeza kwa niaba ya mwelekeo huu, kwa kusaidiwa na waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa. Wanaweza kusaidia kwa kuwashawishi wadau wa nchini humo kuhusu busara ya kuhakikisha kwamba mienendo inayotekelezwa inakuwa ya haki na isiyoegemea upande wowote. Waangalizi wa kura wa nchini siku hizi huwa na wajibu unaoendelea, mara nyingi kwa kufanya kazi na waangalizi wa kimataifa ili kutoa uangalizi na ulinzi wa kuhakikisha uhalali wa uchaguzi.