Usajili wa wapigakura wasiotambulika pia hujulikana kama usajili wa wapigakura kapa. Ni zoezi la kuweka majina ya watu kwenye orodha ya wapigakura hivi kwamba majina au maelezo mengine kuwahusu (k.m. anwani) hayajitokezi kwenye nakala iliyochapishwa au kusambazwa ya orodha ya wapigakura. Katika visa vingine, halmashauri ya kusimamia uchaguzi hutoa nafasi ya usajili wa wapigakura wasiotambulika kwa kuunda na kutunza orodha tenge ya wapigakura kapa.
Wapigakura wanaweza kutaka kutotambuliwa kwa sababu mbalimbali. Pengine ile ya kawaida ni kwamba wamehujumiwa nyumbani au wana hofu kwamba majina yao yakijitokeza huenda kukatatiza usalama wao wa kibinfasi. Vivyo hivyo, wahanga wa makosa ya jinai wanaweza kuhofia kwamba mtu fulani aliyetekeleza uovu huo akiachiliwa huru kutoka jela atajua jinsi ya kuwapata na kulipiza kisasi.
Katika kuwahakikishia watu hao usajili wa kutoonyesha maelezo kuwahusu, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kudhihirisha uwajibikaji wake kwa hatua ya kutimiza hilo. Isitoshe, huaminika kwa mapana kwamba watu hawapaswi kunyimwa haki zao za kidemokrasia kwa sababu ya kusumbuliwa na dhuluma za kinyumbani au makosa ya jinai. Kwa wakati huo, usajili unaoficha taarifa kuhusu watu walioomba kufanyiwa hivyo unaonekana kutolingana na kanuni ya uwazi na uangavu wa mchakato wa uchaguzi. Angaa katika nadharia, orodha kapa inaweza kuwa njia kusababisha udanganyifu mkubwa katika uchaguzi ikiwa idadi kubwa za watu zinahusika na hivyo orodha hiyo haiwezi kuangaliwa kama kawaida na raia, vyama vya kisiasa au mawakala wake.
Kama ilivyo katika masuala mengi ya usimamizi wa uchaguzi, suluhisho bora liko katikati ya usawazisho kati ya haja ya usiri wa idadi ndogo ya watu na sababu halali za kutotaka kutambulika na haja ya uwazi na uangavu katika usimamizi wa uchaguzi. Halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kuhitaji mtu mwingine yeyote anayetaka kuwekwa kwenye orodha ya wapigakura kapa kutoa ushahidi kwamba kutambuliwa kwao kunaweza kuhatarisha uasiri na usalama wao. Halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza pia kutoa orodha hiyo ya wapigakura kapa ili ikaguliwe na idadi ndogo ya mawakala wa vyama vya kisiasa watakaokuwa wamekiri kwa kuapa kudumisha usiri wa orodha hiyo.