Udanganyifu katika uchaguzi huchukua maumbo mbalimbali. Katika visa vingine, unaweza kutekelezwa na raia wenyewe au katika makundi maalumu; katika visa vingine unaweza kutekelezwa na serikali kwa nia ya kughushi matokeo ya uchaguzi. halmashauri ya kusimamia uchaguzi inapaswa kuwa na uhuru wa kuhakikisha viwango vya usawa katika kukabiliana na udanganyifu katika uchaguzi unaotekelezwa na raia, na kutoa hakikisho kwamba serikali haitatumia udanganyifu pia.
Udanganyifu katika uchaguzi unaotekelezwa na watu binafsi
Kujifanya mtu mwingine. Umbo linalojitokeza sana kuhusu udanganyifu katika ni hali ya kujaribu kupiga kura mara zaidi ya moja, ama kwa kuchukua kadi ya pili ya utambulisho wa mpigakura au kujidai kuwa mpigakura mwingine. Adhabu za kujidai kuwa mtu mwingine au kujisajili mara mbili mara nyingi hutokezwa wazi katika sheria ya uchaguzi; ni pamoja na faini, kufungwa jela au vyote viwili.
- Kupiga kura kwa kutumia jina la watu waliofariki. Kibadala cha kujidai kuwa mpigakura mwingine ni jaribio la kupiga kura zaidi ya mara moja, kwanza kwa kutumia kitambulisho chao wenyewe kupiga kura na kisha kutumia kitambulisho cha mtu aliyefariki. Aina hii ya udanganyifu inaweza kuzuiwa kwa kusasaisha orodha za wapigakura na kuhakikisha kwamba majina ya watu waliofariki yanaondolewa punde. Faini zinaweza kutumiwa kama kizuizi dhidi ya udanganyifu huu.
- Udanganyifu katika kura zilizotumwa kwa njia ya barua. Katika mfumo unaoruhusu upigaji kura wa kutuma kura kwa njia ya barua, kuna hatari kwamba kura hiyo inaweza kuombwa au kujazwa na mtu mwingine tofauti na mpigakura stahifu. Uaminifu wa kura unaweza kutunzwa kwa kuzuia mtu yeyote kuomba kura kwa niaba ya mtu mwingine, aliyepewa jukumu la kuthibitisha utambulisho wa mpigakura, na adhabu kubwa kuwekewa watu wanaovunja kanuni hizi.
Udanganyifu katika uchaguzi unaotekelezwa na makundi au serikali
- Kuzidisha hesabu ya (kuhesabu vibaya)kura. Njia moja ya kuiba kura ni kwa kuhesabu kura vibaya au kujaza sanduku la kura ambazo hazikupigwa kihalali. Hatua mvbalimbali zinaweza kutumika kuzuia vitendo hivi vya udanganyifu: kuruhusu maofisa wa kusimamia uchaguzi peke yao kuingiza kura katika masanduku ya kura; kutumia masanduku angavu ya kupigia kura; na kuhesabu kura machoni pa wawakilishi wa vyama vya kisiasa pamoja na vilevile waangalizi binafsi wa nchini na wa kimataifa, watakaothibitisha uhuru wa mchakato huo wa uchaguzi.
- Vitisho. Wale wanaoazmia kushawishi matokeo ya uchaguzi wanaweza kujihusisha na shughuli za kutisha wapigakura dhidi ya kujisajili au, ikiwa wamesajiliwa, dhidi ya kupiga kura kwenye siku ya uchaguzi.vitisho vinaweza wakati mwingine kuwa vigumu kutambuliwa kwa sababu ya maumbo mbalimbali ambayo hali hiyo inaweza kuchukua, za wazi na za kutumiwa na umma na vile vile kuwa ngumu kueleza.
Hata hivyo, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inahitajika kujua juhudi zinazofanywa za kutisha wapigakura. Inaweza kusaidiwa kwa kuhimiza umma kuripoti visa hivyo vya vitisho kwake. Inaweza pia kufanya kazi kwa ushirikiano na mashirika ya kuhudumia raia na waangalizi wa kitaifa na wa kimataifa wa uchaguzi huo ili kuchunguza visa vya vitisho.
- Kutojumuishwa katika orodha ya wapigakura. Ili uchaguzi uwe wa huru na haki, uchaguzi huo hauna budi kuruhusu wapigakura wote wanaoafiki vigezo vya ustahifu kutokeza mapendeleo yao kwa kupiga kura. Majaribio yanaweza kufanywa ili kuyatenga makundi mengine ya raia kutoka kwenye orodha ya wapigakura, hasa ikiwa wanajulikana kuunga mkono chama fulani cha kisiasa. Halmashauri ya kusimamia uchaguzi inahitajika kufahamu mipango ya majaribio kama hayo na kuhakikisha kwamba hayafaulu. Hatari itakayokuwepo ni kwamba katika kujaribu kujumuisha kundi fulani la watu walio kwenye orodha ya wapigakura, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kuchukuliwa kama inayojaribu kushawishi matokeo ya uchaguzi kuwa ya kuwafaa.