Fomu za usajili wa wapigakura hujitokeza katika maumbo na mitindo mbalimbali. Wakati mwingine wapigakura wengine hujisajili kwa njia ya mtandao na fomu hiyo huwepo tu kama faili ya kielektroniki. Wakati mwingine ni fomu ya karatasi tu ambayo huwekwa kwenye tovuti ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi japo zinapaswa kuchukuliwa, kuchapishwa, kujazwa kwa mikono, na kurudishwa ama kibinafsi au kupitia huduma ya posta. Wakati mwingine ni fomu ya karatasi tu kutoka kwa jhalmashauri ya kusimamia uchaguzi au shirika jingine linalotekeleza jukumu la kusambaza. Na wakati mwingine fomu hiyo inapaswa kujazwa sio tu na mpigakura bali na msajili, mfanyakazi katika kituo cha usajili au ofisa mwingine kama huyo.
Ikiwezekana na katika hali halisi, halmashauri za kusimamia uchaguzi zinaweza kuchagua fomu ya usajili wa wapigakura iliyo na sehemu nyingi za kuraruliwa. Sababu moja ya hili ni kwamba mtindo huu wa fomu unaweza kujumuisha kadi ya utambulisho wa mpigakura, kutenganishwa na kupewa mpigakura huyo baada ya kukamilisha mchakato wa usajili. Kadi hiyo inaonyesha jina na anwani ya mpigakura huyo, tarehe ya uchaguzi, kituo cha kupigia kura na muda wa shughuli hiyo na (katika visa vingine) nambari ya utambulisho wa mpigakura. Taarifa za kibinafsi kwenye kadi hiyo iliyokatwa hulingana na taarifa iliyo kwenye sehemu iliyohifadhiwa na halmashauri ya kusimamia uchaguzi.
Sifa mbalimbali za kiusalama zinaweza kujengwa katika fomu nyingi za usajili wa wapigakura. Kwa mfano, nambari ya usajili inaweza kuchapishwa kwenye sehemu iliyohifadhiwa na halmashauri ya kusimamia uchaguzi na vilevile kwenye kadi hiyo ya kipande kilichokatwa (uwekaji nambari husaidia maofisa kuangalia usambazaji wa fomu hizo). Sehemu zote mbili zinaweza kuwa na picha na ishara za vidole vya mpigakura huyo. Maeneo mengine huhitaji sahihi za shahidi mmoja au zaidi, na wapigakura waliosajiliwa, wanaojitolea kuwa mashahidi wa watu wengine wanaojaza fomu za usajili wa wapigakura.
Suala jingine la kiusalama ni ezeko la tabaka; hili hulenga kuikinga kadi ya usajili ya mpigakura dhidi ya kuharibika. Tabaka hilo linaweza kuwekwa ama kwa kutumia mitindo ya karatasi zenye joto au baridi kutegemea hali ya eneo hilo.
Fomu zenye sehemu nyingi zinaweza kurahisisha utumizi deta kwa ushirikiano. Kwa mfano, kutoa ripoti ya mabadiliko ya anwani kwa ofisi ya posta, mtu mwingine anaweza kuijaza fomu hiyo katika nakala mbili au tatu. Nakala moja ya fomu hiyo hupelekewa halmashauri ya kusimamia uchaguzi hivyo basi kusasaisha vilivyo taarifa kuhusu mpigakura.