Usajili wa wapigakura huhusisha shughuli ambazo zinaweza kufaidika kutokana na matumizi ya teknolojia – kwa mfano, kurekodi na kuhifadhi majina na maelezo mengine ya utambulisho wa kibinafsi (anwani, uraia, umri, jinsia na kadhalika); kuchapisha orodha, wakati mwingine kwa kutumia kigezo cha uteuzi wa watu wengi; kuchunguza mabadiliko katika taarifa za watu baada ya muda; au kugawana deta na mshirika mengine ya serikali. Matumizi muhimu na pana ya teknolojia kwa usajili wa wapigakura ni kutumia tarakilishi katika kuhifadhi orodha za wapigakura. Japo teknolojia nyingine zimeteuliwa ili kuimarisha mfumo wa usajili wa wapigakura, zikiwemo zifuatazo:
- Kuunganisha tarakilishi. Deta ya usajili wa wapigakura inaweza kuingizwa katika tarakilishi tenge, japo upeo mzuri wa matumizi ya tarakilishi ni uwezo wa kuwasiliana na kubadilishana taarifa kwa kutumia tarakilishi zilizounganishwa kwa mitandao. Kwa mfano, tarakilishi katika kituo au ofisi ya usajili huunganishwa pamoja, na kuunganishwa pia na ofisi za kimaeneo na/au za kitaifa. Deta ya usajili wa wapigakura inaweza kukusanywa katika kiwango cha kieneo, ambako inatiwa katika faili za kielektroniki na kisha kuhamishiwa kwenye makao makuu ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi ili kujumuishwa katika rejista kamili ya kitaifa. Hatimaye, makao makuu yanaweza kuzirudisha deta za kiwango cha kituo cha kupigia kura hadi kwenye ofisi za maeneo ili zichapishwe kama orodha za wapigakura.
- Teknolojia ya kugawana deta. Hasa katika maeneo yanayotumia orodha endelevu, halmashauri ya kusimamia uchaguzi hujadiliana kuhusu ushirikiano na mashirika mengine ya serikali ili kugawana mabadiliko katika taarifa za raia binafsi. Kila mdau anaweza kutumia kiziodeta tofauti. Halmashauri ya kusimamia uchaguzi hivyo basi inapaswa kujenga au kununua teknolojia ya kuiwezesha kusoma na kutumia deta kutoka kutoka kwenye viziodeta mbalimbali.
- Upigaji picha za kidijitali hurahisisha kazi ya kujumuisha picha za wapigakura kwenye orodha ya wapigakurana/ au kadi za utambulisho wa wapigakura.
- Utumizi alama za vidole kidijitali umeimarisha ubora na kupunguza gharama ya uwekaji wa alama hizo, ambazo ni kipengele muhimu cha usalama.
- Utabakishaji wa kadi ya utambulisho wa wapigakura unaweza kutatiza majaribio ya kubadilisha taarifa inayopatikana kwenye kadi hiyo, hivyo kusaidia kupunguza udanganyifu wa wapigakura. Tabaka hilo linaweza kuwekwa kwa kutumia karatasi moto au baridi. Utabakishaji baridi ni muhimu hasa kwa matumizi katika vituo visivyo na umeme.
- Unukulishi wa stakabadhi asilia (vyeti vya kuzaliwa, pasi na kadhalika) huruhusu halmashauri ya kusimamia uchaguzi kuweka rekodi ambazo zitathibitisha wazi utambulisho wa mpigakura. Unukulishi pia hupunguza nafasi za mahali ambazo zingehitajika katika kuhifadhi rekodi.
- Uwepo wa intaneti unaibukia kuwa kitu cha lazima kwa mashirika ya umma. Kwenye tovuti yake, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kutundika taarifa kuhusu shughuli zake na vilevile nyenzo za kutumiwa kwa shughuli ya elimu kwa wapigakura.
Teknolojia inayoweza kuwa na umuhimu mkubwa kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi ipo kwa wingi. Aidha, kilichopo katika jumuia ya usimamizi wa uchaguzi ni ujuzi na tajriba ya kutosha katika kutathmini bidhaa na huduma zilizoko katika mazingira ya matumizi. Ushauriano na wenzao unaweza kuwa na manufaa makubwa katika kuamua iwapo itakuwa bora kutumia teknolojia tofautui tofauti au kupendekeza matumizi yake kwa serikali.