Usajili wa wapigakura mara nyingi huwa kitu cha lazima katika kupiga kura. Ili waweze kutokeza mitazamo yao katika mchakato ya demokrasia, raia hawana budi kusajiliwa. Halmashauri za kusimamia uchaguzi mara nyingi hufanya kampeni za kusajili makundi ya watu ambayo hayana uwezekano wa kushiriki katika uchaguzi, kama vile vijana, wanawake, watu maskini au wale kutoka makabila yanayodunishwa. Zoezi hili huzua maswala mengi ya muhimu: je, halmashauri ya kusimamia uchaguzi ina jukumu la kuhakikisha kwamba ushiriki katika uchaguzi ni wa hali ya juu au kupunguza au unalenga kupunguza tofauti katika viwango vya kushiriki vya makundi mbalimbali ya watu? Je, badala yake linapaswa kuwa jukumu la wakereketwa wa chama fulani cha kisiasa kutafuta kura wakati wa uchaguzi?
Wasimamizi wa uchaguzi wana mitazamo mablimbali kuhusu suala hili. Kwa wengine, kuhakikisha kwamba wapigakura wanajikeza kwa wingi ni moja katika majukumu yao ya kimsingi. Inafuatia kwamba watu wengi iwezekanavyo wajumuishwe kwenye orodha ya wapigakura na wanapaswa kuwakilisha kwa upana idadi ya watu. Wasimamizi wa uchaguzi wanaoshikilia mtazamo huu huenda wakatumia shuguli za usajili uanolenga wapigakura fulani, na kuunda mipango ya elimu kwa wapigakura inayolenga kuongeza ufahamu na uhusishwaji wa watu wote wa jumuia fulani katika siasa zao.
Mtazamo mwingine kinyume na huu ni kwamba wasimamizi wa uchaguzi wanapaswa kutoa nafasi ya kushiriki bali si shinikizo kwa yeyote kuchukua nafasi hiyo. Yaani, wajibu wa halmashauri ya kusimamia uchaguzi kimsingi ni kutoa nafasi sawa kwa raia wote, kuelekeza jumbe zake kwa umma kwa jumla na kuhakikisha kwamba shughuli za kuwasajili wapigakura zinakuwepo kwa wapigakura wote watarajiwa. Wale wanaopendekeza mtazamo huu huchukulia kwamba wao ni wasimamizi wa uchaguzi wasioegemea upande wowote na hivyo wanapaswa kuonekana kama wasio na mapendeleo. Kampeni ya usajili unaolenga, au juhudi ya kushiriki kwa wapigakura wengine japo si wote, inaweza kuwa na athari ya kusaidia makundi mengine kushinda mengine. Ikiwa hiyo ndiyo hali, hatua yoyote ile huhujumu uhuru wa kisiasa wa halmashauri ya kusimamia uchaguzi.
Hili ni suala tata na hakuna jibu moja linaloweza kuwa sahihi kwa wasimamizi wote wa uchaguzi na katika hali zote. Pale inapowezekana, ni muhimu kuweka wazi kanuni zinazoongoza utendakazi wa halmashauri ya kusimamia uchaguzi ili badiliko katika uongozi lisilete mabadiliko ya ghafla katika shughuli zake.