Baada ya kukusanya deta ya usajili kwenye fomu za usajili wa wapigakura, maofisa wa kusimamia uchaguzi wanaweza kuto orodha ya mwanzo ya wapigakura. Hii hupewa vyama vya kisiasa na wagombea ili waitumie katika kampeni zao. Halmashauri ya kusimamia uchaguzi huitumia kukadiria idadi ya watu wanaostahili kupiga kura katika kila eneo la kijiografia; kadirio hilo husaidia katika kuweka maeneo pana ya upigaji kura. Isitoshe, wapigakura wanaweza kukagua taarifa zao kama zinavyojitokeza katika orodha ya kwanza ya wapigakura, na wanaweza kushtaki madai au malalamishi kwa nia ya kuyabadilisha au kuyaongeza kwenye orodha hiyo.
Katika siku za awali, orodha za mwanzo za wapigakura zilibandikwa ili umma uweze kuzikagua au kuwekwa katika sehemu za kuingiwa na umma, kama vile ofisi za serikali au maktaba za umma. Hofu kuhusu usiri imesababisha nchi nyingi kukoma kuzitoa orodha hizo wazi. Badala yake, aina fulani ya ukaguzi (k.m. postikadi) kwa kawaida hupewa au kutumwa kwa wapigakura ili kuthbitisha kwamba wamesajiliwa na kueleza kule wanakopaswa kupiga kura. Katika maeneo mengine, wapigakura wanaweza kukagua hali zao za usajili kwa kwenda kwenye ofisi za halmashauri ya kusimamia uchaguzi wenyewe, kuwasiliana na halmashauri hiyo kwa njia ya simu au kufikia tovuti yake.
Orodha ya kwanza huwawezesha wananchi kukagua iwapo wamesajiliwa ipasavyo ili kuweza kupiga kura katika uchaguzi unaofuata au kuhitaji kuwasiliana na ofisi ya usajili kuomba mabadiliko katika orodha yao. Orodha hiyo opia huviruhusu vyama vya kisiasa na wagombea kutambua iwapo kuna maelezo mengine yasiyo linganifu au yana kasoro, na ikiwa wengi katika wafuasi wao hawakusajiliwa na wanapaswa kuhimizwa kuomba nafasi ya kusajiliwa.
Ikiwa maofisa wa kushughulikia usajili hawapokei mabadiliko yoyote, orodha ya kwanza inabadilika na kuwa orodha ya mwisho ya wapigakura ya kutumiwa kwenye siku ya uchaguzi. Matokeo haya yatakuwa ya kushtusha, hata hivyo, kwa kuwa hakuna uwezekano kwamba maofisa hao walifaulu kuwasiliana na kila mpigakura mstahifu katika awamu ya kwanza ya usajili. Maombi ya kawaida kuhusu mabadiliko hupokewa, hivyo basi kuwezesha matumizi ya orodha ya kwanza kama msingi wa kutathmini jinsi mchakato wa usajili ulivyofanya kazi katika misingi ya usasa, ulinganifu na ukamilifu. Mabadiliko ya muhimu hujumuishwa ili kutoa orodha iliyosasaishwa ya wapigakura (k.v. ya mwisho).
Orodha ya mwanzo ya wapigakura pia hutekeleza angaa majukumu mawili:
- Kabla orodha ya mwisho kuwa tayari, halmashauri ya kusimamia uchaguzi huvipa vyama orodha ya wapigakura ambao vinaweza kuwasiliana nao katika eneo la kupigia kura, jimbo la uchaguzi au eneo pana la uchaguzi.
- Katika nchin nyingine hutoa msingi wa kupiga hesabu ya ufadhili ambao serikali itampa kila mgombea au chama, na vilevile idadi ya pesa za kutumiwa wakati wa kampeni yenyewe.
Wajibu wa Vyama vya Kisiasa
Orodha ya mwanzo ya wapigakura kwa kawaida hutolewa kwa vyama vya kisiasa ili viweze kuipitia – ukaguzi wa ziada kuhusu ubora wa orodha hiyo. Vyama vya kisiasa vina haja ya kibinafsi katika ukaguzi wa orodha na kuthibitisha ulinganifu wake. Kushiriki kwao katika mchakato wa usajili wa wapigakura ni muhimu:
- Chaguzi huru na za haki huhitaji uwazi na uangavu. Yaani, hakuna taarifa yoyote ya muhimu inayopaswa kuwekwa siri. Kwa kugawana orodha za mwanzo za wapigakura na vyama vya kisiasa, usimamizi wa uchaguzi hukuza uangavu wa mchakato wa uchaguzi.
- Ili kuimarisha ubora wa orodha, wasimamizi wa uchaguzi mara nyingi hujaribu hutaka usaidizi wa wapigakura na mashirika ya kijamii ya kushughulikia raia. Vyama mara nyingi vinaweza kutoa taarifa mpya na masahihisho kwenye taarifa zilizoorodheshwa. Matokeo yake yatakuwa orodha itakayofanya kazi vizuri katika misingi ya usasa, ulinganifu na ukamilifu.
Masuala kuhusu Usiri
Ukaguzi wa nje kuhusu orodha haupaswi kuhujumu usiri wa watu walioorodheshwa. Katika nchi nyingine, hofu nyingi kuhusu kutunzwa kwa usiri zimeibuliwa kuhusiana na taarifa na taratibu za usajili wa wapigakura. Sababu za kibinafsi kuhusu usalama zinaweza kuhitaji kwamba majina ya baadhi ya wapigakura waliosajiliwa yabanwe ili yasionekane katika rejista inayofikia umma; mifano ni majaji, maofisa wa polisi, na watu wanaohofia kuvamiwa na wachumba walioachana nao pale awali. Watu kama hao wanaweza kuwekwa kwenye orodha ya wapigakura wasiotambulika au kapa.
Wakati mwingine ni taarifa fulani tu iliyotiliwa mipaka inayoweza kuwepo ili kusomwa na nafsi za tatu, yaani, yeyote mwingine kando na halmashauri ya kusimamia uchaguzi au raia mwenyewe. Maeneo mengine huweka mipaka dhidi ya kuonyesha wazi nambari za utambulisho wa raia au vitambulisho vingine; wengine hawatokezi umri au anwani za makazi. Maeneo mengi hufunga matumizi ya orodha hizo kwa matumizi mengine yasiyo ya uchaguzi;kwa hasa, hukataza matumizi yake kwa faida za kibiashara ili kuhakikisha kwamba watu wanaojisajili kupiga kura hawazuiwi kunufaika kutokana na matoleo fulani ya kimauzo.
Orodha ya Kwanza na Mifumo Mbalimbali ya Usajili
Katika kutayarisha orodha ya mwanzo, kuna tofauti kubwa kati ya utaratibu katika mfumo unaotumia orodha ya muda na mfumo unaotumia rejista endelevu: wakati ambapo shughuli hii inafanywa. Katika mifumo mingine inayotumia orodha ya muda, halmashauri ya kusimamia uchaguzi hutengeneza orodha ya kwanza katika kipindi rasmi cha uchaguzi kwa kuanza shughuli ya usajili. Katika mfumo unaotumia orodha endelevu, halmashauri ya kusimamia uchaguzi hukamilisha sehemu kubwa ya kazi ya kutengeneza orodha ya mwanzo mapema kabla ya kuanza kwa kampeni ya uchaguzi; ikiwa kazi hiyo ilifanywa vizuri (yaani, kuafiki vigezo vitatu vya usasa, ulinganifu na ukamilifu), kunapaswa kuwa na mabadiliko kiasi kwenye orodha hiyo wakati wa kipindi cha uchaguzi. Wasimamizi wa uchaguzi hufafanua njia hii ya utendakazi kama “njia ya kukimu gharama ya ziada.” Bila shaka, si shughuli za ziada zinazoweza kuondolewa kutoka kwenye mchakato wa usajili wa wapigakura – isipokuwa katika nchi inayotumia mfumo wa sajili ya raia.
Katika mfumo kama huo hakuna haja ya kuwa na orodha ya mwanzo ikiwa sajili imekuwa ikitengenezwa na kutunzwa vizuri. Mara nyingi huwa lazima kwa raia kuorodheshwa katika sajili ya raia, na taarifa iliyomo inaweza kutumiwa kwa majukumu mbalimbali, ikiwemo uchaguzi. Kwa kawaida usajili huhitajika wakati wa kuzaliwa au kupewa uraia; hivyo basi, raia wanapaswa kuripoti vilivyo mabadiliko kwenye taarifa yao ya usajili – kwa mfano, mabadiliko ya jina, makazi au hadhi ya kindoa. Orodha hiyo hivyo basi husasaishwa mara kwa mara na kuwekwa katika usasa kila mara. Kwa sababu hiyo, hakuna haja ya orodha ya mwanzo ya wapigakura pale uchaguzi unapoitishwa.