Wakati wa kupanga mfumo wa uchaguzi, ni bora kuanza na orodha ya vigezo ambavyo hujumlisha yale ambayo unapanga kutimiza, yale unataka kupigana nayo na, kwa mapana zaidi vile ambavyo unataka serikali iwe katika viwango vya bunge na utawala. Kigezo ambacho hufuata hushughulikia maeneo mengi, lakini orodha haijakamilika, na msomaji anaweza kuongeza baadhi ya vitu ambavyo ni muhimu pia. Ni kweli kwamba baadhi ya kategoria huingiliana na huweza kukinzana. Haya ni kwa sababu kawaida hukinzana: na ni kawaida ya mpango wa kitaasisi kwamba usawazishaji lazima ufanywe kati ya matamanio na malengo yenye ushindani. Safu hizi kimsingi hulenga kwenye kigezo cha miundo na sio mpango wa malengo wenyewe. Mchakato wa mpango hushughulikiwa kwa kina katika sehemu zake za Mchakato wa Mabadiliko na Ushauri kwa Mipango ya Mifumo ya Uchaguzi.
Kwa mfano, mtu anaweza kutoa nafasi kwa wagombeaji huru kuchaguliwa, na wakati huo huo kuhimiza maendeleo ya vyama vya kisiasa vilivyo imara. Au, wapangaji wa mifumo ya uchaguzi huweza kuonelea kama bora zaidi kuunda mfumo ambao utawapatia wapigaji kura uwanja mpana wa uteuzi kati ya vyama na wagombeaji, lakini hili huweza kufanya karatasi ya kura kuwa changamano zaidi jambo ambalo linaweza kuwa ngumu kwa wapigaji kura wasio na elimu ya kutosha. Ujanja wa kuteua (au kurekebisha) mfumo wa uchaguzi ni kupanga vigezo kulingana na umuhimu wake kisha kutathmini ni mfumo upi wa uchaguzi, au mchanganyo wa mifumo, ni bora zaidi katika kufanikisha malengo haya.
Mada ndogo za sura hii:
- Kutoa Uwakilishaji
- Kufanya Uchaguzi kuwa wa Kufikiwa na wenye Maana
- Kutoa Motisha kwa kusudi la Mapatano
- Kuwezesha Serikali Imara na yenye Ufanisi
- Kuhakikisha Serikali Inawajibika
- Kuhakikisha Wawakilishaji Wanawajibika
- Kuvipa Moyo Vyama vya Kisiasa
- Kuimarisha Uwakilishaji na Usimamizi wa Upinzani
- Kufanya Mchakato wa Uchaguzi Kufanikiwa na wa Kudumu
- Kuhakikisha Viwango vya Kimataifa Vinazingatiwa
- Vigezo vya Upangaji: Hitimisho

