Uwakilishaji huweza kuchukua kwa kiasi maumbo manne.
Kwanza, uwakilishaji wa kijiografia humaanisha kuwa kila eneo, liwe ni mjini au mji mkuu, au mkoa au wilaya ya uchaguzi, lina wanachama wa uanabunge walioteuliwa na ambao watawajibikia eneo lao.
Pili, migao ya kiitikadi katika jamii huweza kuwakilishwa katika bunge, iwe ni katika uwakilishaji kutokana na vyama vya kisiasa au uwakilishaji huru au yote mawili.
Tatu, wanabunge wanaweza kuwakilisha hali ya kisiasa ya chama ambayo ipo nchini hata kama vyama vya kisiasa havina misingi ya kiitikadi. Ikiwa nusu ya wapigaji kura watapigia kura chama kimoja lakini chama hicho kinashindwa, au kutopata hata kiti kimoja katika bunge, basi mfumo huo utachukuliwa kuwa hauwezi kuwakilisha mapendeleo ya watu.
Nne, dhana wa uwakilishaji wa kujieleza huchukulia kuwa uanabunge unastahili kuwa kwa kiwango kikubwa ‘kioo cha taifa’ ambayo inastahili kutazama, kuhisi, kufikiri na kutenda kwa njia inayoakisi watu kwa kujumla. Bunge ambalo linajitosheleza katika kujieleza hujumlisha wanaume na wanawake, vijana na wazee, matajiri na maskini, na kuangaza madhehebu mbalimbali ya kidini, kijamii, kilugha na makundi ya kikabila yaliyo katika jamii.

