Uchaguzi wote huwa mzuri na bora, lakini huweza kuwa na umuhimu kidogo kwa watu ikiwa itakuwa vigumu kwao kupiga kura au ikiwa mwishowe mitazamo yao ya kwamba kura zao hazitakuwa na athari yoyote kuhusiana na jinsi serikali inavyoendeshwa. Utulivu wa kupiga kura hutegemea maswala kama vile uchangamano wa karatasi ya kura, wepesi wa mpigaji kura wa kufika katika eneo la upigiaji kura, ikiwa orodha ya majina ya wapigaji kura imejumlisha majina yote, na kiwango cha kujiamini cha mpigaji kura kwamba kura yake itakuwa ya siri.
Uhusika katika uchaguzi – kwa kiasi kama uteuzi wa hiari - pia huweza kuongezeka wakati matokeo ya uchaguzi, ama katika kiwango cha kitaifa au katika eneo la mpigaji kura, yanaonekana kuwa muhimu kwenye serikali itakayochaguliwa. Ikiwa unajua kwamba mgombeaji uliyemchagua hana nafasi ya kujinyakulia kiti katika wilaya fulani, vichocheo vya upigaji kura ni gani? Katika baadhi ya mifumo ya uchaguzi, kura zilizoharibika ( yaani kura halali kwa wagombeaji wanaopoteza, ikilinganishwa na karatasi za kura ambazo huondolewa kutokana na idadi ya jumla) huweza kutoa kiwango kikubwa cha kura zote za taifa.
Mwisho, uwezo halisi wa taasisi itakayochaguliwa husaidia kuamua ikiwa uchaguzi wake utakuwa na umuhimu wowote. Uchaguzi mtupu katika mifumo ya utawala wa mabavu hutoa uteuzi usio wa ukweli, pale ambapo bunge zilizopo huwa na athari kidogo kwenye uundaji wa serikali au kwenye sera za serikali, huwa hazina umuhimu ikilinganishwa na uchaguzi wa uanabunge ambao huwa na uwezo wa kuamua elementi muhimu katika maisha ya watu ya kila siku.
Hata katika mifumo yenye demokrasia, uteuzi wa mfumo wa uchaguzi huweza kuathiri uhalali wa taasisi. Kwa mfano, katika Australian Senate kati ya mwaka wa 1919 hadi 1946 iliyochaguliwa na mfumo wa uchaguzi uliokosa usawazishaji kwa kiwango cha juu (Alternative Vote katika wilaya zenye uanachama wa zaidi ya mmoja) ambao matokeo yake yaliegemea upande mmoja na kukosa uwakilishaji wa kutosha. Hili lilipelekea kupuuza uhalali halisi wa Senate yenyewe kulingana na maoni ya wapigaji kura pamoja na wanasiasa na pia kulingana na mitazamo ya wakaguzi, hili lilipuuzilia mbali ufuasi wa umma kuhusiana na taasisi za serikali ya shirikisho kwa ujumla. Baada ya kufanyia mabadiliko mfumo ili kupata mfumo uliosawazishwa kwa kiwango fulani (Mfumo wa Single Transferable Vote), mwaka wa 1948, Senate ilianza kutazamwa kama yenye kuaminika na yenye kutoa uwakilishaji na hivyo heshima na umuhimu wake kuongezeka katika utoaji wa uamuzi.

