Mifumo ya uchaguzi huweza kutazamwa sio tu kama njia ya kuunda taasisi za uongozi bali kama mikakati ya kusuluhisha migogoro katika jamii. Mifumo mingine katika hali zingine, huweza kutolea motisha vyama ili viweze kutoa maombi ya ufuasi wa uchaguzi nje ya maeneno yao ya kuchaguliwa: kwa mfano, hata kama chama kitapata ufuasi kutoka kwa wapigaji kura waafrika, mfumo fulani wa uchaguzi huweza kuupa kichocheo cha kuweza kutumika katika eneo la wazungu au wapigaji kura wengine. Hivyo, msingi wa sera za chama cha kisiasa huweza kukosa uamuzi kamili na kamilifu na pia wenye kuunganisha na kujumuisha. Vichocheo sawa vya mfumo wa uchaguzi huweza kuvifanya vyama kukosa ujumuishi wa kikabila, kimaeneo, kilugha au kiitikadi. Mifano ya jinsi mifumo ya uchaguzi imfanya kazi kama vyombo vya kusuluhisha migogoro imetolewa katika makala haya.
Kwa kutazama upande wa pili, mifumo ya uchaguzi huweza kuhimiza wapigaji kura kutafuta nje ya makundi yao na kufikiria kupigia kura vyama ambavyo hapo awali vimekuwa vikiwakilisha makuni tofauti. Mienendo kama hii ya upigaji kura huweka nafasi ya kukubalika na ujenzi wa jamii. Mifumo ambayo humpa mpigaji kura zaidi ya kura moja katika kuorodhesha wagombeaji kulingana na upendeleo wake hutolea mpigaji kura nafasi ya kutoka nje ya mipaka ya kijamii iliyowekwa. Katika makubaliano ya uchaguzi wa Ijumaa Kuu huko Nothern Island, kwa mfano, uhamishaji wa kura chini ya mfumo wa STV uliwafaidi ‘vyama vilivyokuwa vinatetea amani’ huku vikitoa matokeo yenye usawa kwa kiwango cha juu. Katika uchaguzi wa mwaka wa 2003, hata hivyo, badiliko la kura za uteuzi wa pendeleo la kwanza kwenye vyama uliokuwa umekita mizizi ulionekana kuwa na athari kama hizo.

