Matarajio ya serikali imara na yenye ufanisi hayatoi uamuzi na mfumo wa uchaguzi pekee, lakini matokeo yanayotokana na mfumo huweza kuchangia uwepo wa uthabiti kuhusiana na mitazamo mbalimbali.
Maswali muhimu ni:
- Ikiwa wapigaji kura huchukukulia mfumo kuwa wa haki,
- Ikiwa serikali inaweza kutoa sheria na kutawala, na
- Ikiwa mfumo utakwepa ubaguzi dhidi ya baadhi ya vyama ua makundi yanayohusika.
Matarajio ya ikiwa matokeo yatakuwa halali au la hutofautiana kwa mapana kutoka nchi moja hadi nchi nyingine. Mara mbili huko United Kingdom (UK) (kati ya mwaka wa 1951 na 1974) chama kilichoshinda kura nyingi zaidi nchini kote kilishinda viti vichache kuliko upinzani, lakini hili lilichukuliwa kuwa mabadiliko ya ghafla katika mfumo uliotekeleza kazi vizuri kuliko ukosefu wa haki wa moja kwa moja ambao unahitaji kubadilishwa. Kwa upande mwingine, matokeo kama hayo hayo huko New Zealand katika mwaka wa 1978 na 1981, ambapo National Party ilichukua tena uongozi kinyume na kwamba kilishinda viti vichache kuliko chama cha upinzani cha Labour, inasifiwa kama mwanzo wa miondoko ya mabadiliko ambayo yalileta mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.
Swali la ikiwa serikali inayotawala inaweza kuweka sheria kwa ufanisi hunasibishwa kwa kiasi na ikiwa itaweza kuleta pamoja kundi la wengi wanoaweza kufanya kazi katika bunge, na hili pia hunasibishwa na mfumo wa uchaguzi. Kama kanuni ya jumla iliyoko, mifumo ya uchaguzi yenye ufuasi wa wengi huwa na uwezo wa kutoa bunge ambapo chama kimoja huweza kushinda upinzani ukiwekwa pamoja, ambapo mifumo ya PR inaweza kutoa serikali ya muungano. Hata hivyo, ikumbukwe kuwa mifumo ya PR huweza pia kutoa chama kimoja chenye ufuasi wa wengi na mifumo ya wengi huweza kukosa kuacha hata chama kimoja kikiwa na wafanyakazi walio wengi. Mengi hutegemea muundo wa mfumo wa chama na hali ya jamii yenyewe.
Mwisho, mfumo unastahili kwa vyovyote vile kufanya kazi kwa njia ya uchaguzi isiyo na upendeleo kwa vyama vyote na wagombeaji; haustahili kubagua kwa uwazi dhidi ya kundi lolote la kisiasa. Mtazamo kuwa siasa za uchaguzi katika demokrasia ni uwanja wa mwenye nguvu mpishe ni ishara kwamba mpangilio wa kisiasa ni dhaifu na kwamba ukosefu wa uthabiti hauko mbali. Mfano mzuri wa haya ni katika uchaguzi wa mwaka wa 1998 huko Lesotho ambapo chama cha Lesotho Congress for Democracy kilishinda kila kiti katika bunge huku kikiwa na asilimi 60 ya kura zote chini ya mfumo wa FPTP. Hali ya ukosefu wa amani iliyofuata, ilisababisha kuingilia kati kwa wanajeshi nchini kupitia Southern African Development Community, ulidhihirisha kuwa matokeo ya aina hii hayakuwa tu yenye kukiuka haki bali yenye hatari, na mfumo wa uchaguzi ulibadilishwa ili kutumika katika uchaguzi wa baadaye.

