Uwajibikaji ni mojawapo ya misingi ya serikali yenye uwakilishaji. Ukosefu wake huweza kuhitaji ukosefu wa utulivu wa muda mrefu. Mfumo wa kisiasa wenye uwajibikaji ni ule ambao huwa na serikali ambayo inawajibikia wapigaji kura katika viwango vya juu kabisa. Wapigaji kura wanastahili kuwa na uwezo wa kuathiri serikali katika jinsi inavyoendesha mambo, ama kwa kubadilisha miungano ya vyama vilivyo uongozini au kutoa katika uongozi chama kimoja ambacho kinashindwa kutekeleza majukumu yake. Mifumo ya uchaguzi iliyoundwa vizuri huwa na uwezo wa kutekeleza lengo hili.
Kaida ya hekima katika nyanja hizi huwa sahili. Hapo awali, mifumo ya wengi kama vile FPTP ilichukuliwa kama yenye kutoa chama kimoja kikichukua uongozi, huku mifumo ya PR ilinasibishwa na miungano ya vyama vingi. Huku wazo pana na unasibishaji huu likisalia kuwa halali, kumekuwa na mifano tosha katika miaka ya hivi karibuni katika uchaguzi wa FPTP yenye kutoa baraza la wanachama kutoka vyama tofauti (kwa mfano Afrika Kusini) ili kuongeza kiwango cha uaminifu kuhusu machukulio ya moja kwa moja kwamba mfumo mmoja wa uchaguzi utatoa aina fulani ya serikali. Kwa uwazi, mifumo ya uchaguzi huwa na athari kubwa kwenye maswala ya utawala katika mifumo ya uraisi na ya uanabunge.

