Uwajibikaji katika kiwango cha kibinafsi ni uwezo wa wapigaji kura kukagua kwa ufanisi wale ambao wamechaguliwa, wanaokiuka ahadi walizoweka wakati wa kampeni au kutoweza au kuwa wazembe ofisini na ‘kutupa wahuni nje’. Mifumo mingine hutilia mkazo jukumu la wagombeaji wa eneo fulani waliojulikana zaidi, kuliko wale walioteliwa na vyama imara. Mifumo ya wengi imekuwa ikitazamwa kama yenye kuzidisha uwezo wa wapigaji kura wa kutoa wawakilishaji binafsi wasiojimudu. Tena hili wakati mwingine hubakia kuwa halali. Hata hivyo, uhusiano unakuwa dhaifu pale ambapo wapigaji kura hujitambulisha mwanzo na vyama kuliko kujitambulisha na wagombeaji, kama ilivyo huko UK. Wakati huo huo, mifumo ya orodha wazi na huru pamoja na STV hupangwa ili kuwaruhusu wapigaji kura kuwa na uteuzi wa mgombeaji wanaompenda katika muktadha wa mfumo wa usawazishaji.

