Uzito wa ushahidi kutoka demokrasia mbili mpya hupendekeza kuwa demokasia za muda mrefu zilizounganishwa – yaani, kiasi ambapo demokrasia ya mfumo wa utawala huwa umekingwa kutokana na changamoto za kinyumbani kwenye udhabiti wa mpangilio wa kisiasa, na hivyo mfumo wa uchaguzi unahitaji kuhimiza haya kuliko kuimarisha usarambatikaji wa chama.
Ili kufanya hili, mifumo ya uchaguzi huweza kusingiziwa hasa kutenga vyama vyenye ufuasi wa viwango vidogo au vya wastani. Maendeleo ya majukumu ya vyama kama chombo cha viongozi binafsi wa kisiasa ni mkondo mwingine ambao unaweza kutekelezwa au kukwamizwa na maamuzi ya upangaji wa mfumo wa uchaguzi. Wataalamu wengi pia hukubali kuwa mfumo wa uchaguzi unastahili kuhimiza maendeleo ya vyama ambavyo vina miegemeo ya maadili mapana ya kisiasa pamoja na mipango mahususi ya sera, kuliko shughuli finyu za kikabila, kirangi au kimaeneo. Pamoja na kupunguza tishio la migogoro ya kijamii, vyama ambavyo huwa na mitazamo hii ya ‘migawanyo iliyoenea’ huwa na uwezekano wa kuakisi maoni ya taifa kuliko vile ambavyo vina mitazamo inayotawaliwa na mahitaji ya kiufuasi au kimaeneo.

