Utawala wenye mafanikio hutegemea sio tu wale ambao wako katika uongozi lakini, kwa wingi, wale ambao huwapinga na kuwakagua. Mfumo wa uchaguzi unastahili kusaidia katika kuhakikisha uwepo wa kundi imara la upinzani ambao unaweza kutathmini kwa karibu bunge, kuuliza kuhusu utendakazi wa serikali, kuchunga haki za wachache, na kuwakilisha waliowachagua kwa ufanisi.
Makundi ya upinzani yanastahili kuwa na wawakilishaji wa kutosha ili yafanikiwe (ikichukuliwa kwamba utendakazi wao katika uchaguzi unahakikisha hivyo) na katika mfumo wa uanabunge unastaahili kuwakilisha kibadala halisi katika serikali iliyoko. Hakika uwezo wa upinzani hutegemea mambo mengine mengi bali na utuzi wa mfumo wa uchaguzi, lakini ikiwa mfumo wenyewe huufanya upinzani kutoweza kufanya chochote, uongozi wa kidemokrasia hudhoofishwa mwanzoni.
Sababu kuu ya badiliko hili la mfumo wa uchaguzi wa MMP huko New Zealand ni ukosefu wa uwakilishaji wa vyama vidogo chini ya FPTP. Wakati huo huo, mfumo wa uchaguzi unastahili kuzuia maendeleo ya mwelekeo wa ‘mshindi ndiye huchukua kila kitu’ ambao huwafanya viongozi kutotazama maoni ya wengine na mahitaji ya wapigaji kura wa upinzani na huona uchaguzi na serikali kama kinyang’anyiro kisicho na umuhimu.
Katika mfumo wa uraisi, raisi anahitaji ufuasi wa kutegemewa wa kundi kubwa la wanabunge; hata hivyo, jukumu la wengine la kupinga na kukagua mapendekezo ya uongozi serikalini pia huwa muhimu. Ugawanyaji wa utawala kati ya bunge na serikali kwa usawa hutoa jukumu la ufuatiliaji wa karibu wa serikali kutoka kwa wanabunge wote, sio tu upinzani pekee. Hili huwa muhimu katika kutoa wazo la elementi za mfumo wa uchaguzi ambao hujishughulisha na umuhimu wa vyama vya kisiasa na wagombeaji ukiwepo uhusiano kati ya vyama na wanachama waliochaguliwa.

