Mwisho, mpango wa mifumo ya uchaguzi leo hutekelezwa katika maeneo ya muktadha wa makubaliano ya kimataifa, maafikiano na njia nyingine za vyombo vya kisheria zinazoathiri maswala ya kisisasa.
Huku kukiwa hakuna kanuni hata moja ya viwango vya kimataifa vya uchaguzi ianyokubalika, kuna makubaliano kuwa viwango kama hivi vijumuishwe:
- Kanuni za uchaguzi ulio huru, wa haki na unaofanywa baada ya kipindi fulani ambao huhakikisha haki ya kupiga kura ya kila mtu mzima,
- Siri wakati wa uchaguzi na uhuru dhidi ya ushurutishaji, na
- Uwajibikaji kwenye kanuni ya mpigaji kura mmoja, kura moja.
Zaidi ya hayo, huku kukiwa hakuna masharti ya kisheria kuwa mfumo fulani wa uchaguzi unapendelewa zaidi ya mwingine, kuna ongezeko la utambuzi wa masuala muhimu ambayo huathiriwa na mifumo ya uchaguzi, kama vile uwakilishaji wa haki kwa wananchi wote, usawa kati ya wanawake na wanaume, haki za walio wachache, kuzingata mahitaji ya walemavu, n.k.
Haya hufanywa kuwa ramsi katika vyombo vya kimataifa vya kisheria kama vile katika mwaka wa 1948 kwenye Universal Declaration of Human Rights pamoja na 1966 kwenye International Covenant on Civil and Political Rights, na katika makubaliano na wajibu unaohusu demokrasia unaofanywa na mashirika ya kieneo kama vile European Union (EU) pamoja na Organization for Security and Co-operation in Europe (OSCE), Organization of American States (OAS), Council of Europe (COE) na Commonwealth.

