Ni jukumu la wanaoleta mabadiliko, sio tu katika kuelewa muundo wa kisheria wa mijadala ya kiufundi na athari za mabadiliko yanayowezekana bali pia kuelewa na waweze kueleza mijadala ya kisiasa na athari za muundo mpana wa kisiasa wa nchi. Sauti muhimu za wateteaji, wasomi, na wanahabari huweza kuchangia katika kukuza utambuzi wa wa umma kwamba mabadiliko ni muhimu. Lakini idadi ya kutosha ya wale walio mamlakani itahitaji kuthibitishiwa faida, zikiwemo faida watakazopata.
Pamoja na mvuto uliopo na unaozidi kuongezeka katika mifumo ya uchaguzi idadi ya watu, waliosoma na jamii kwa jumla ambao huelewa athari zinazowezekana za mabadiliko huweza kuwa haba. Haya hutatizwa zaidi na ukweli kuwa jinsi mifumo ya uchaguzi inavyoendeshwa huweza kutegemea zaidi maelezo machache ya wanaoleta mabadiliko wanahitaji sio tu kufanya kazi kabisa na kueleza habari za kisheria ambayo inaweza kuwa muhimu katika kutekeleza mabadiliko, bali pia kuunda mipango na masingizio ya kiufundi (kawaida wakitumia data kutokana na uchaguzi uliotangulia) ili kuonyesha, kwa mfano, umbo na athari za mapendekezo kwenye wilaya za uchaguzi au athari zinazowezekana kuhusu uwakilishaji wa vyama vya kisiasa. Masingizio ya kiufundi huweza pia kutumika ili kuhakikisha kuwa matukio yote ya dharula yameshughulikiwa na kutathmini matokeo dhahiri yasiyotarajiwa; ni bora kujibu maswali wakati mbapo mabadiliko yanapoimarishwa kuliko katikati mwa migogoro baadaye.
Kwa hakika, sio athari zote za mfumo wa uchaguzi zitakazojulikana mapema . Ni kweli kwamba kupanga mfumo wa uchaguzi wakati hakuna uwazi wa jinsi matokeo yatakavyokuwa kulingana na kura halisi na ugawanyaji wa viti huweza kuwa muhimu inapofikia wakati wa kuafikiana kuhusu mfumo ambao utaonekana kuwa wa haki zaidi kwa wote wanaohusika .
Maelezo ya kiufundi na athari za kimitambo zinastahili kufahamika zaidi iwezekanavyo kwa wote na kueleweka mapema ili kuleta mabadiliko. Mipango ya kuboresha mpigaji kura, kwa mfano, kuwaalika wanachama kutoka kwa umma ili kushiriki katika majaribio ya uchaguzi chini ya mfumo mpya unaopendelewa, huweza kuwavutia wana habari na kuongeza ufahamu pakiwepo mapendekezo ya mabadiliko. Pia wanaweza kusaidia kutambua matatizo – kwa mfano, ugumu wa mpigaji kura mwenye kadi za kupiga kura - ambazo mfumo mpya unaweza kuzalisha.

