Wapigaji kura, viongozi katika uchaguzi, wanasiasa na watangazaji wote huonekana kutosheka na yale wanayoyafahamu. Miaka mingi ya matumizi ya mfumo mmoja imesawazishwa vikwazo vyote vya mifumo iliyowekwa. Mfumo mpya hivyo basi huweza kutazamwa kama hatua kuelekea kusikojulikana, na matatizo wakati marekebisho huweza kutokea kutokana na kutojulikana kwake. Haya hayawezi kuepukwa kabisa na wapangaji wa mabadiliko ya uanabunge au uwakilishi yanayowekwa. Mchakato wa mabadliko ni mihimu ikiwa tu mipango ya elimu ya wapigaji kura itatiliwa mkazo ili kueleza washiriki wote jinsi mfumo mpya unavyofanya kazi pamoja na mpango na makubaliano ya kanuni za marekebisho zinazowapendeza wote.
Elimu ya wapigaji kura iliyofanikiwa zaidi –pamoja na elimu ya viongozi wa uchaguzi –huchukua muda na hivyo ni muhimu ianzishwe mapema. La kusikitisha ni kwamba, hakika muda huwa hautoshi kwa baraza linaloongoza uchaguzi linapopanga uchaguzi chini ya mfumo mpya , lakini haistahili kuwa ikiwa mpango mzuri unafuatwa. Wapatanishi wote wazuri hutumia wakati uliobanwa kabla ya makubaliano ya mwisho kufikiwa na hili ni kweli wakati mfumo mpya ni matokeo ya majadiliano magumu kati ya washiriki wa kisiasa . EMB iliyofanikiwa huweza hata hivyo kuandaa mengi zaidi na kwa mapema zaidi.

