Kanuni za mfumo wa wafuasi wengi ni sahihi. Baada ya kura kupigwa na kuhesabiwa , wagombeaji au vyama vyenye kura zaidi hutangazwa washindi (panaweza kuwa na masharti zaidi). Hata hivyo, njia ya kufanikisha haya hutofautiana katika mambo mengi.
Aina tano za mifumo yenye wafuasi wengi ni kama vile:
- First Past the Post(FPTP)
- Block Vote (BV)
- Party Block Vote(PBV)
- Alternative Vote (AV)
- Two Round System (TRS)
Katika mfumo wa FPTP (wakati mwingine ukiitwa mfumo wa wengi ulio na uanachama mmoja wilayani) mshindi ndiye mgombeaji mwenye kura nyingi lakini haimaanishi idadi kamili ya kura. Mfumo huu unapotumika katika wilaya zenye uanachama zaidi ya mmoja, huchukuliwa kama Block Vote. Wapigaji Kura huwa na kura nyingi kama vilivyo viti vya kujazwa , na wagombeaji walio na idadi kubwa ya wapigaji kura hujaza nafasi pasipo kutilia maanani asilimia ya kura watakazopata. Mfumo huu pamoja na mabadiliko kwamba wapigaji kura hupigia kura vyama badala ya wagombeaji binafsi huchukuliwa kama Party Block Vote.
Mfumo wa wafuasi wengi kama vile Alternative Vote na Two Round System, hujaribu kuhakikisha kwamba mgombeaji aliyeshinda, hupokea idadi kamili ya wingi (yaani, asilimia 50). Kila mfumo kimsingi hutumia chaguo la pili la wapigaji kura ili kupata mshindi aliye na idadi kamili ya wafuasi wengi ikiwa yeye hujitokeza katika awamu ya kwanza ya upigaji kura.


Variants of the Alternative Vote