Urazini unaotegemezwa kwenye mifumo ya PR ni mgao wa chama katika kura ya taifa na mgao wake wa viti bungeni; ikiwa chama kikubwa kitashinda asilimia 40 ya kura zote, kinastahili kushinda karibu asilimia 40 ya viti, na chama kidogo kikiwa na asilimia10 ya kura kinastahili kupata asilimia 10 ya viti bungeni. Ulinganifu huu kati ya mgao wa kura wa chama na mgao wake wa viti hutoa vichocheo kwa vyama vyote kuunga mkono na kushiriki katika mfumo.
PR huhitaji kutumia wilaya za uchaguzi zenye zaidi ya uanachama mmoja; haiwezekani kugawa kiti kimoja kilichochaguliwa kwenye kikao kimoja kwa usawa. Kuna aina mbili za mfumo wa PR - List PR na single Transferable vote (STV). Usawa huchukuliwa kuwa wenye kutimizwa kupitia matumizi ya orodha ya chama, pale ambapo vyama vya kisiasa hutoa orodha ya wagombeaji kwa wapigaji kura katika kiwango cha kitaifa au kimaeneo, lakini uchaguzi wa upendeleo huweza kufanikiwa pia: Single Transferable Vote, pale ambapo wapigaji kura hupanga wagombeaji katika wilaya za uanachama zaidi ya mmoja, ni mfumo mwingine unaotumiwa na uliosawazishwa.
Kuna masuala mengine muhimu ambayo yanaweza kuwa na athari kuhusu jinsi mfumo wa PR hufanya kazi katika utendakazi wake. Jinsi idadi ya wawakilishaji wa kuchanganuliwa ilivyo kubwa kutoka wilaya fulani, ndivyo mfumo wa uchaguzi utakavyokuwa wa kiwango cha juu. Mifumo ya PR pia hutofautiana katika mawanda yake ya uteuzi yanayotolewa mpigaji kura - iwe mpigaji kura atachagua kati ya vyama vya kisiasa, wagombeaji binafsi au wote.

