Kama mfumo wa SNTV, mfumo wa Limited Vote ni mfumo wa wafuasi wengi unaotumiwa katika wilaya zenye uanachama zaidi ya mmoja. Tofauti na mfumo wa SNTV, wapigaji kura huwa na zaidi ya kura moja – lakini kura chache kuliko wagombeaji waliojitoa kuchaguliwa. Hesabu yake huwa inalingana na ile ya SNTV, huku wagombeaji wenye idadi kubwa ya kura zilizopigwa wakishinda viti. Mfumo huu hutumiwa katika uchaguzi mwingi wa kiwango cha kimaneneo, lakini utumiaji wake katika kiwango cha taifa umetumiwa katika nchi za Gibraltar na Spain, ambapo umekuwa ukitumika kuchagua chemba cha juu huko Spain tangu mwaka wa 1977. Katika hali hii, huku kukiwa na wilaya zenye uanachama zaidi ya mmoja, kila mpigaji kura huwa na kura moja chini zaidi kuliko idadi ya wanachama watakaochaguliwa.

