Kama katika mfumo wa SNTV, LV ni sahili kwa wapigaji kura na rahisi kupiga hesabu. Hata hivyo, unapelekea kutoa matokeo yenye ukosefu wa usawazishaji kuliko katika SNTV. Nyingi ya mijadala inayohusu mashindano ya ndani ya chama, uongozi wa chama, na siasa zenye miegemeo ya wateja hutumika katika mfumo wa LV kwa njia inayolingana na ile ya SNTV.

