Umuhimu na udhaifu wa Borda Count huwa na ulinganifu na ule wa mifumo mingine ya uchaguzi wa upendeleo. Wapigaji kura huweza kudhihirisha seti ya kina ya upendeleo, lakini kwa upande mwingine mfumo unahitaji kwa kiasi kiwango kidogo cha kuweka hesabu ili kufanya kazi, na huweza kuwa vigumu kwa wapigaji kura kuelewa. Kiwango cha usawazishaji na idadi ya kura zilizoharibika kitategemea zaidi ukubwa wa wilaya.

