Mfano mzuri na wa mwisho wa mpango wa mfumo wa uchaguzi ni ule wa Borda Count ulioboreshwa na unaotumika katika eneo ndogo la nchi ya Pacific huko Nauru. Mfumo wa Borda Count hupendelewa kama mfumo wa uchaguzi ambapo wapigaji kura huorodhesha wagombeaji kama ilivyo katika mfumo wa Alternative Vote. Unaweza kutumika katika wilaya zenye uanachama wa zaidi ya mmoja. Huwa kuna hesabu moja pekee, hakuna kutolewa katika orodha na upendeleo huhesabiwa kama ‘kura za kiwango fulani’ katika mfumo wa Borda Count ulioboreshwa na ulioasisiwa huko Nauru, pendeleo la kwanza linahitaji hesabu moja, la pili linahitaji hesabu nusu na la tatu linahitaji thuluthi moja, n.k. Haya huwekwa pamoja na mgombeaji au wagombeaji wenye idadi ya juu ya kura hutangazwa washindi.

