Kanuni za uchaguzi huweza kuathiri maeneo mengi tofauti yanayohusiana na jinsi wanachama katika nchi fulani wanavyowakilishwa. Nyingi ya athari hizi huwa ni matokeo ya moja kwa moja kuhusu uteuzi wa mfumo wa uchaguzi wenyewe, huku vingine vitatokana na mpango ulio wazi wa mambo yaliyoongezwa kwenye katiba au sheria za uchaguzi.

