Kuna njia nyingi ambazo huwezesha uwakilishaji wa wanawake. Mifumo iliyosawazishwa huonekana kuwa na uchaguzi wa wanawake zaidi, kimsingi kwa kuondoa dosari za kiasili zilizo bayana katika mifumo ya FPTP ya uhitaji wa kuwakilisha mgombeaji mmoja ‘anaye kubalika zaidi’. Mifumo ya uchaguzi ambayo hutumia kwa kiasi fulani wilaya kubwa kiidadi huhimiza vyama kuteua wanawake katika misingi ambapo tikiti zilizo sawa zitaongeza nafasi zao za kuchaguliwa. Baadhi ya nchi zinazotumia List PR pia huhitaji wanawake kuunda kiwango fulani cha wagombeaji walioteuliwa na kila chama.
Pamoja na uteuzi wa mfumo wa uchaguzi. Pia kuna Mikakati mwingine ambayo huweza kutumiwa kuongeza idadi ya wanawake katika uwakilishaji.
- Kwanza, kuna viti vilivyotengwa, pale ambapo idadi fulani ya viti hutengewa wanawake bungeni. Viti hivi hujazwa na ama wawakilishaji kutoka maeneo au kutokana na vyama vya kisiasa huku vikiwa na usawazishaji wa moja kwa moja na mgao wao kamili wa kura ya kitaifa . Viti vilivyotengwa kawaida huwa katika mifumo yenye wafuasi wengi na kawaida huwa vimeingizwa kwenye katiba ya nchi. Huko India, viti kuhusu utawala wa mikoa, katika baadhi ya maeneo huwa vimegawanywa katika makundi matatu. Katika kila uchaguzi, wanawake pekee wanaweza kuteuliwa kuwakilisha kundi moja la viti, hivyo kuhakikisha kiwango cha chini thuluthi moja ya wanawake watakaochaguliwa
- Pili, sheria za uchaguzi huweza kuhitaji vyama vya kisiasa kutoa idadi fulani ya wagombeaji wanawake katika uchaguzi. Hili hutokea zaidi katika mifumo ya uchaguzi ya PR, kwa mfano huko Namibia (asilimia 30 ya wagombeaji katika kiwango cha chini). Pia inahitajika katika kipengele cha List PR huko Bolivia katika mfumo wa MMP (asilimia 30 ya wagombeaji). Hata hivyo, sheria hazihakikishi kila wakati kwamba lengo litaafikiwa isipokuwa tu pale ambapo kuna sheria zilizowekwa na mikakati iliyotolewa inayohakikisha kuwa wanawake wamewekuwa katika nafasi za kuchaguliwa kwenye orodha za chama (yaani, nafasi katika orodha ya chama ambayo huwezekana ikichukuliwa kwamba idadi ya kura za chama zinazotarajiwa, na zinazohitajika kuwa katika tume ya uwakilishaji wa chama).
- Tatu, vyama vya kisiasa huweza kutafuta quota zao za ndani za wanawake kama wagombeaji bungeni. Huu ni mkakati wa kawaida kabisa unaotumiwa kuinua kiwango cha uhusika wa wanawake katika maisha ya siasa, na umewahi kutumika katika viwango tofauti kwa ufanisi duniani kote: na ANC huko Afrika Kusini, na Peronist Party nd Radical Civic Union (UCR) huko Argentina, CONDEPA (Conscience of the Fatherland) huko Bolivia, chama cha Democratic Revolution (UCR) huko Mexico pamoja na vyama vya Labour huko Australia na UK na kote Scandinavia. Matumizi ya uteuzi wa wagombeaji wanawake pekee na Labour Party katika uchaguzi wa UK mwaka wa 1997 karibu usababishe idadi maradufu ya wanawawake bungeni kutoka 60 hadi 119. Katika mwaka wa 2004 nchi 14 zilizokuwa na quota ziliwekwa kwenye katiba , nchi 32 zilikuwa na quota zilikuwa zimetolewa kwenye bunge, na kulikuwa na nchi 15 kwenye mifumo ya uchaguzi iliyochanganywa na nchi 45 katika mifumo ya PR. Nchi mbili ‘nyingine’ - Afghanistani na Jordan – walitumia quota.
Mifumo ambayo huhakikisha uwakilishaji wa wanawake katika bunge hutofautiana pale ambapo ufanisi wao na athari/ matokeo yao yanavyohusika . Kwa mfano, viti vilivyotengwa huweza kusaidia uhakika kwamba wanawake hupata nafasi ya kuchaguliwa katika ofisi, lakini baadhi ya wanawake hujadili kuwa quota huishia kuwa njia ya kuwafurahisha na hatimaye kuwatenga wanawake au kuwapatia hadhi wanawake wa ukoo wa jamii fulani na marafiki wa wanasiasa wanauume wa hapo awali kuliko kuwahimiza wanawake kukuza kazi zao katika siasa , jambo ambalo huweza kuchukua miaka mingi. Kwa kuwa njia ya kuingia katika siasa kwa kawaida hufanywa katika kiwango cha chini na hata na wanasiasa wanaume, inaweza kuwa na mahusiano zaidi katika kuanzisha quota, mwanzoni katika kiwango cha chini kuliko katika kiwango cha taifa.
Uwezo wa kuchaguliwa bungeni haumaanishi uwezo wa kupewa uwezo fulani wa kufanya uamuzi , na katika baadhi ya nchi wanawake wawakilishi, hasa wale waliochaguliwa kutokana na viti vilivyotengwa au vya hadhi tofauti hutengwa kutokana na majukumu ya ufanyaji uamuzi. Huku katika nchi nyingine, wanawake wametumia nafasi walizopewa kutoa mchango muhimu wa hapo awali kuhusina na uundaji wa sera.

