Sio bunge zote ambazo huwa na chemba kimoja, hasa katika nchi kubwa kieneo, nyingi huwa na mabunge mawili. Ulimwenguni kote, karibu thuluthi mbili ya nchi zote huwa na bunge moja huku thuluthi moja ikiwa na mabunge mawili.
Nyingi ya vyemba vya pili (kawaida vikiitwa bunge la Malodi au senate) huwepo kutokana na sababu moja au mbili. Sababu ya kwanza ni kutoa mwakilishaji wa aina tofauti au kuwakilisha mahitaji tofauti, kawaida uwakilishaji wa maeneo au wilaya za chini. Sababu ya pili ni kufanya kazi kama chemba cha kupitia mambo upya ili kutoa kipindi cha mapumziko au uchelewaji dhidi ya maamuzi muhimu kwenye bunge la chini. Uwezo wa chemba cha juu huwa mdogo ikilinganishwa na uwezo wa bunge la chini hasa pale ambapo kuna mabunge ya kupitia mambo upya.
Miundo ya mabunge mawili hutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine, lakini kawaida matumizi ya kimsingi ya bunge la pili ni katika mifumo ya shirikiso ili kuwakilisha sehemu ndogo za shirikisho. Kwa mfano, mataifa ya Marekani Brazil na Australia, Lander huko Ujerumani, na katika wilaya huko Afrika Kusini huwa zimejitenga katika bunge la juu. Kwa mfano, hili huhusisha upendeleo kwenye mataifa au wilaya ndogo kwa sababu hili hupelekea kuwepo kwa usawa katika uwakilishaji kati ya mataifa haya. Pamoja na haya, mabunge mengi ya pili huwa na uchaguzi uliotawanywa; thuluthi moja ya bunge huchaguliwa kila baada ya miaka miwili huko USA na India, n.k.
Baadhi ya nchi ambazo mabunge yao ya juu ni, ‘mabunge ya kupitia mambo upya’ huwekewa vikwazo maalum. Huko Thailand, kwa mfano, Senate sasa hivi huchaguliwa, lakini maseneta hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha kisiasa au hata kufanya kampeni za uchaguzi. Aina moja ya uwakilishaji wa hiari ambayo haitumiki sana ni matumizi ya bunge la juu kimakusudi ili kuwakilisha makundi fulani ya kikabila, kilugha, kidini au kitamaduni. Bunge la pili kwa pia huweza kuwa na wawakilishi wanaotetea haki za kibinadamu. Huko Malawi, kwa mfano, katiba huruhusu maseneta 32 kutoka kwa maseneta 80 kuchaguliwa kutokana na orodha ya wagombeaji walioteuliwa na makundi ya kijamii yenye shughuli za pamoja. Makundi haya hutambuliwa kama mashirika ya akina mama, walemavu, makundi ya utoaji huduma za afya na elimu, sekta za biashara na kilimo, vyama vya wafanyakazi, watu mashuhuri katika jamii, na viongozi wa kidini. Bunge la Malodi la Uingereza ambalo hukashifiwa sana hutetewa mara kwa mara katika misingi kwamba huwa lina watu wenye taalama fulani kuhusu sera na pia wana uwezo wa kukagua uundaji wa sheria zinazopendekezwa na wanasiasa bungeni katika serikali. Vile vile, bunge la pili katika nchi kama vile Fiji na Botswana hutumiwa kuwakilisha machifu wa kitamaduni, hata kama hawa huwa wameteuliwa katika awamu ya kwanza na kuchaguliwa katika awamu ya pili.
Kwa sababu ya tofauti hizi, nyingi ya mabunge ya pili huwa kwa kiasi fulani yamechaguliwa, kwa njia ya moja kwa moja au hawajachaguliwa. Kati ya wale waliochaguliwa, mamlake yake mengi ni kuakisi majukumu tofauti ya mabunge mawili kwa kutumia mifumo tofauti ya uchaguzi kwenye bunge la juu na kwenye bunge la chini. Huko Australia, kwa mfano, bunge la chini huwa limechaguliwa kupitia mfumo wa walio wengi (AV) huku bunge la juu, ambalo huwakilisha mataifa mbalimbali, huchaguliwa kupitia mfumo wa usawazishaji (STV). Hili humanisha kuwa mapendekezo ya wachache ambayo kwa kawaida hayawezi kuwa na uwezo wa kushinda uchaguzi kwenye bunge la chini bado wana nafasi ya kupata uchaguzi, katika miktadha ya uwakilishaji wa kitaifa, kwenye bunge la juu. Huko Indonesia, bunge la chini huchaguliwa kupitia mfumo wa List PR, huku bunge la juu likitumia mfumo wa SNTV kuchagua wawakilishaji wanne kutoka kila wilaya. Huko Columbia, huku mabunge yote mawili yakichaguliwa kupitia mfumo wa PR, Seneta huchaguliwa kutoka wilaya zote nchini, na hivyo kuwezesha vyama vidogo na mapendeleo ya walio wachache kuwakilishwa bungeni.

