Mfumo wowote wa uchaguzi uliotajwa katika sehemu hii huweza kutumika katika kiwango cha serikali ya eneo au wilaya, lakini kawaida huwa na mambo fulani ambayo huzingatiwa kutokana na jukumu mahususi la serikali za mitaa. Hususan, kwa sababu serikali za mitaa huhusu maswala ya kimsingi na rahisi ya kila siku, uwakilishaji wa kijiografia kwa kawaida hupewa kipa umbele.
Wilaya zenye uanachama mmoja huweza kutumiwa ili kutolea kila ujirani nafasi ya kusema kuhusu maswala yao, hasa pale ambapo vyama vya kisiasa huwa dhaifu au havipo. Pale ambapo wilaya hizi ni ndogo, kawaida huwa zaidi na sifa moja. Hili kwa kawaida hutazamwa kama jambo nzuri, lakini ikiwa tofauti katika serikali za mitaa itahitajika, kanuni ya ‘spokes of a wheel’ ya uwekaji wa wilaya itahitajika. Hapa mipaka ya wilaya sio tu mizunguko ambayo huchorwa kwenye ujirani unaotambulikana lakini ni sehemu za mizunguko ambayo huwa na kitovu cha mji mkuu na kuishia katika viungani vya mji huo. Hili humaansha kwamba wilaya moja hujumlisha wapigaji kura kutoka katika maeneo ya mji na viungani vyake, na huwa ni mchanganyiko wa tabaka la wafanyakazi na la kikabila.
Kwa kulinganua, mitaa katika baadhi ya nchi hutumia mifumo ya PR kwa sababu serikali za mitaa huwa na wilaya zenye orodha moja ya PR ambayo huweza kuakisi kwa usawa maoni yote tofauti ya kisiasa kwenye mtaa huo. Ili kufanikisha hili, hata hivyo, nafasi maalum huhitaji kuwekewa wawakilishaji wa mashirika wa mitaa ambao hawana misukumo yenye mitazamo ya vyama vya kisiasa ya kuteua orodha, na pengine ya walio huru kuteuliwa kama orodha ya mtu mmoja.
Pia ni kweli kuwa mfumo wa uchaguzi wa mtaani huweza kuwa kama sehemu ya masikizano yanayohusu mfumo wa ubunge. Kwa mfano, katika baadhi ya nchi zenye demokrasia changa kama vile Congo (Brazzaville) na Mali, utamaduni na athari za Ufaransa zimesababisha uwepo wa Two-Round System katika bunge, huku matamanio ya kuwa pamoja na pia kuakisi zaidi uaminifu wa kimaeneo na kikabila ukisababisha uteuzi wa PR katika uchaguzi wa mitaa.
Mjadala kati ya uanabunge na uraisi katika katiba za nchi huwa na kifanani katika kujadili muundo wa serikali ya mtaa. Serikali zinazochaguliwa kwa njia ya moja kwa moja na mameya ambao huongoza miji mikuu ambayo huwa imejitenga na bunge la uwakilishaji lililochaguliwa kimaneo zinaendelea kuwa nyingi zaidi dunia, huku zikipuuza uongozi uluiochagulia na miundo ya kamati ya pamoja ambayo inatoa huduma kwa njia ya moja kwa moja. Mifumo ambayo ipo ya kucahgua magavana na mameya hakika inafanana na ile ya uchaguzi wa uraisi wa moja kwa moja, na usambamba huweza kutolewa pia wakati wa kuzingatia maswala yanayozunguka mahusiano kati ya mfumo wa uchaguzi na uhusiano kati ya bunge na mawaziri katika kiwango cha nchi.

