Aina mbalimbali za mifumo ya uchaguzi huweza kuhimiza aina tofauti za mpangilio wa vyama na mfumo wa chama. Huku ikiwa muhimu kwa mifumo ya vyama kuwa na uwakilishaji iwezekanavyo, wataalamu wengi hupendelea mifumo ambayo huhimiza maendeleo ya vyama yenye miegemeo ya maadili na imani pana ya vyama na sera maalum za mipango, kuliko kuwa na shughuli finyu za kikabila, kirangi, au kieneo. Pamoja na kupunguza hatari za migongano ya kijamii, vyama ambavyo huwa vimehusishwa na ‘migawanyo mipana inayopatikana kote’ huweza kuakisi maoni ya kitaifa kuliko ile ambayo ina misingi yake hasa kwenye shughuli za ufuasi wa kikundi au kieneo.
Mifumo ya kisiasa yenye makao makuu ya pamoja na ambayo hutumia mfumo wa orodha funge ya PR huwa na uwezo mkubwa wa kuhimiza muungano imara wa chama; na kinyume chake, mifumo iliyotawanya uongozi wilayani kama vile FPTP huweza kuwa na athari zilizo kinyume. Lakini kuna mabadiliko mengine ya uchaguzi ambayo huweza kutumiwa ili kuathiri maendeleo ya mifumo ya vyama.
Kwa mfano, demokrasia changa kama Russia na Indonesia zimejaribu kuunda maendelo ya mifumo mipya ya vyama kwa kutoa vichocheo vya kitaasisi ili kunda vyama vya kitaifa badala ya vile vya kimaneo.
Nchi nyingine kama vile Ecuador na Papua New Guinea zimetumia usajili wa vyama na mahitaji ya ufadhili ili kufanikisha malengo yanayolingana, Upatikanaji wa ufadhili wa kitaifa na /au wa kibinafsi ni swala la kimsingi ambalo hupatikana katika mpango wa mfumo wa uchaguzi, na kawaida kikwazo kikubwa pekee kwenye ujitokezaji wa vyama vipya vya kisiasa vilivyo na uwezo.
Kama ambavyo uteuzi wa chama cha kisiasa utakavyoathiri jinsi ambavyo mfumo wa chama cha kisiasa kinavyokuzwa, mfumo wa chama wa kisiasa uliopo huathiri uteuzi wa mfumo wa uchaguzi. Vyama vilivyopo vina uwezo wa kuunga mkono mabadiliko ambayo yanaweza kuwaathiri kwa njia hasi, au mabadiliko ambayo yanaweza kufungua uwezekano wa vyama vipya pinzani kupata nafasi ya kuingia kwenye mfumo wa chama cha kisiasa, isipokuwa tu pawepo na umuhimu imara wa kisiasa. Mtawanyo wa teuzi za mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi huweza basi kukumbwa na ugumu.
Aina mbali mbali za mifumo ya uchaguzi pia huweza kusababisha mahusiano tofauti kati ya wagombeaji na wafuasi wao. Kijumla, mifumo ambayo hutumia wilaya zenye uanachama mmoja, kama vile mifumo ya walio wengi, hutazamwa kama yenye kuhimiza wagombeaji wa kibinafsi kujiona kama wajumbe kutoka eneo fulani la kijiografia na wenye uwezo wa kuwakilisha mapendekezo wa waliowachagua mashinani. Kwa kulinganua, mifumo ambayo hutumia wilaya zenye uanachama zaidi ya mmoja, huwa na uwezekano mkubwa wa kutekeleza uwakilishaji ambao uaminifu wake wa kimsingi huwa kwenye chama chao kuhusu maswala ya kitaifa. Mitazamo yote miwili huwa na umuhimu ambao ndio sababu ya ongezeko la wingi wa mifumo ilichanganywa ambayo huwekwa pamoja katika uwakilishaji katika kiwango cha kieneo na kitaifa.
Swali la uwajibikaji huulizwa kila wakati katika mijadala ya vyama vya kisiasa na ya mifumo ya uchaguzi hasa kuhusu wanachama wakibinafsi walioteuliwa. Uhusiano uliopo kati ya wapigaji kura, wanachama waliochaguliwa, na vyama vya kisiasa huathiriwa sio tu na mfumo wa uchaguzi lakini pia na mahitaji mengine ya muundo wa sheria za vyama kama vile muda wa kutumikia, mahitaji ya kupima mahusiano kati ya vyama na wanachama wake ambao wawakilishaji waliochaguliwa, au mahitaji yanayowekea vikwazo wanachama waliochaguliwa kubadilisha vyama bila kujiuzuru bungeni.
Uhuru wa wapigaji kura wa kuchagua kati ya wagombeaji kuliko kati ya vyama ni kipengele kingine cha uwajibikaji. Nchi nyingi katika miaka ya hivi karibuni hivyo basi zimeanzisha elementi kubwa ya uchaguzi wenye miegemeo ya mgombeaji, kwa mfano kwa kuanzisha orodha wazi katika mfumo wa uchaguzi wa PR.

