Hakika hali ya, na umuhimu wa elimu kwa wapigaji kura hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine, lakini ikiwa ni wakati wa kuwatolea mafundisho wapigaji kura kuhusu jinsi ya kujaza au kuweka alama kwenye karatasi za kura huwa kuna tofauti bayana kati ya mifumo tofauti. Kanuni ambazo huzingatiwa wakati wa upigaji kura katika mifumo iliyopendelewa kama vile AV, STV an Borda Count huwa changamano zaidi na ikiwa inatumiwa kwa mara ya kwanza elimu kwa umma huhitaji kushughulikia suala hili, hasa ikiwa mpigaji kura anahitajika kuhesabu wagombeaji wote kulingana na jinsi wanavyopendelewa kama ilivyo huko Australia. Ongezeko la matumizi ya mifumo iliyochanganyika, mingi ikiwatolea wapigaji kura karatasi mbili za kura, pia hutoa ongezeko la kiwango cha uchangamano wa wapigaji kura. Kwa kulinganua, kanuni zinazoongoza mifumo ya kura moja kama vile mifumo ya FPTP, PBV au SNTV huwa rahisi kueleweka. Mifumo inayosalia huwekwa kati ya hali hizi mbili zinazokinzana.

