Mifumo ya FPTP, AV, BV, SNTV, orodha ya PR, Borda Count na STV yote huhitaji uchaguzi mmoja pekee kwa siku moja (hata kama ukubwa wa uchaguzi wa FPTP huko India huhitaji kufanywa kwa kipindi cha wiki nne) kama katika mifumo sambamba na MMP. Mifumo ya Awamu mbili huwa ya gharama ya juu na ngumu kuendesha kwa sababu kawaida huhitaji mchakato mzima wa uchaguzi utekelezwa juma moja au majuma mawili baada ya awamu ya kwanza.

