Ikiwa kiti cha uwakilishaji kitaachwa wazi katikati ya vipindi viwili vya uchaguzi, mifumo ya orodha ya PR kawaida hujijaza kwa kutumia mgombeaji wa pili katika orodha akifuata yule aliyeondoka, hivyo basi kuondoa haja ya kufanya uchaguzi mwingine kupitia uchaguzi wa kujaza pengo. Hata hivyo, mifumo yenye ufuasi wa wengi kawaida huwa na nafasi za kujaza viti wazi kupitia uchaguzi wa kujaza pengo. Wakati ambapo mifumo mingine inapotumika mtazamo wowote huweza kutumika; chini ya STV Jamhuri ya Ireland hufanya uchaguzi wa kujaza pengo la viti bungeni, lakini Australi haifanyi hivyo kujaza nafasi za senate. Pia kuna uwezekano wa kuepuka uchaguzi wa kujaza pengo kwa kuchagua wawakilishi badala wakati mmoja na ule wa uchaguzi wa wawakilishi wa kawaida, kama inavyofanyika huko Bolivia. Uchaguzi wa kujaza pengo huwa mdogo na hivyo basi wa gharama ya chini ikilinganishwa na uchaguzi wa kawaida, lakini katika baadhi ya nchi huwa bado wanaweka mzigo mkubwa kwenye bajeti na viti wakati mwingine huachwa wazi kwa muda mrefu kwa sababu ya ukosefu wa uwezo wa kupanga uchaguzi wa kujaza pengo. Hili huwa tatizo kubwa katika baadhi ya nchi huko maeneo ya kusini mwa Afrika ambapo ugonjwa wa ukimwi kawaida hupelekea kuwepo kwa idadi kubwa ya viti vilivyoachwa wazi katikati ya vipindi viwili vya uchaguzi. Katika baadhi ya hali kama hizi, uchaguzi wa kujaza pengo huweza kuwa na athari kubwa ya kisiasa ikilinganishwa na kujaza pengo kwa wanachama binafsi na huonekana kutokea kama mtihani wa katikati ya kipindi cha bunge kuhusu uwajibikaji wa serikali. Pamoja na hayo, ikiwa idadi ya mapengo yanayostahili kujazwa wakati wa kipindi cha ubunge huonekanakuwa muhimu, hili linaweza kusababisha mabadiliko kwenye muundo wa uanabunge na msingi wa uongozi wa serikali ulioteteleka.

