Mifumo ya FPTP, SNTV na orodha funge ya PR iliyo sahili huwa rahisi kuhesabu kwa sababu jumla ya kura moja kwa kila chama au mgombeaji anahitajika kushughulikia matokeo. Mifumo ya BV na LV huhitaji maofisa wa kupigisha kura kuhesabu idadi fulani ya kura kwenye karatasi moja ya kura na mifumo sambamba na MMP kawaida huhitaji kufanya hesabu ya karatasi mbili za kura. Mifumu ya AV, BC na STV kama mifumo inayopendelewa ikihitaji alama kuwekwa kwenye karatasi ya kura huwa changamano kufanyia hesabu.

