Mojawapo ya hitimisho dhahiri inayotokana na utafiti wa ulinganifu wa mifumo ya uchaguzi ni tofauti na matumizi ya teuzi zilizopo. Kawaida, wapangaji na wanaoandika rasimu za miundo ya katiba, ya kisiasa na ya uchaguzi huchagua mfumo wa uchaguzi wanaoufahamu zaidi kawaida katika demokrasia mpya, mfumo wa watawala wa kikoloni waliokuwepo ikiwa walikuwepo – badala ya kufanya utafiti kamili teuzi zilizopo. Wakati mwingine elementi za uwekaji wa amani au misukumo ya nje hushurutisha teuzi zilizopo.
Lengo kuu wa nakala hii ni kutoa baadhi ya maarifa ya kuwa na uamuzi razini utakaofanywa. Haipendekezi tu mabadiliko kamili kwa mifumo ya uchaguzi iliyopo; hakika uzoefu wa ulinganifu wa marekebisho ya uchaguzi kufikia sasa hupendekeza kwamba mabadiliko machache huku yakiboresha sehemu zile za mfumo uliopo na unaofanya kazi vizuri, huwa teuzi bora kuliko kukimbilia kabisa mifumo mipya na isiyofahamika.
Kuna mengi ya kujifundisha kutokana na uzoefu wa wengine. Kwa mfano, nchi yenye mfumo wa FPTP ambayo inapendelea kuhamia kwenye mfumo uliosawazishwa zaidi huku ukisalia na uhusiano wa kijiografia na wanaeneo bunge huweza kutaka kuzingatia uzoefu wa New Zealand, ambao ulitumia mfumo wa MMP mwaka wa 1993, au Lesotho ambao walifanya hivyo mwaka wa 2002. Nchi kama hii ambayo inataka kuweka wilaya za uanachama mmoja lakini unaohimiza nafasi na makubaliano ya mwingiliano wa makundi wanaweza kutathmini uzoefu wa mfumo wa AV katika eneo la Oceania (hasa Fiji au Papua New Guinea). Nchi yoyote ambayo ina migawanyo mikubwa ambayo hupendelea kufanya mabadiliko ya kidemokrasia itahitaji kutolewa ushauri ili kuzingatia sheria yenye makabila mengi ya ugawanyaji wa uongozi, mfumo wa uchaguzi wa orodha PR umewezesha huko Afrika Kusini na zaidi kipindi kirefu cha usumbufu cha Bunge la Ireland kaskazini lililochaguliwa kupitia mfumo STV. Mwisho nchi ambayo hupendelea kupunguza gharama na ukosefu wa utulivu uliosababishwa na mfumo wa TRS wa kumchagua rais huweza kutathmini uteuzi wa mfumo wa AV uliotumiwa na Jamhuri ya Ireland. Katika hali hizi zote, uteuzi wa mfumo wa uchaguzi umekuwa na athari wazi kwenye siasa za nchi husika.
Mwongozo ufuatao hutoa muhtasari wa ushauri unaopatikana katika mada ya sehemu hii:
Hakikisha Kila Kitu ni Sahili na Wazi
Miundo ya mfumo ya uchaguzi yenye ufanisi na kudumu huweza kuwa na uwezekano wa kueleweka kwa urahisi na mpigaji kura pamoja na mwanasiasa. Uchangamano mwingi huweza kusababisha ukosefu wa maelewano, athari zisizotarajiwa na ukosefu wa uaminifu kutoka kwa wapigaji kura kuhusu matokeo.
Usiogope kuwa Mvumbuzi
Mifumo mingi ya uchaguzi iliyofanikiwa inayotumiwa ulimwenguni sasa hivi yenyewe huwakilisha mitazamo yenye uvumbuzi kwa matatizo mahususi na huwa imeboreshwa ili kufanya kazi vizuri. Kuna mengi ya kujifundisha kutokana na uzoefu wa wengine – kutoka kwa nchi jirani na hali tofauti zinazofanana.
Uwe Makini kwa Masuala ya Kimuktadha na Kiwakati
Mifumo ya uchaguzi haiwezi kufanya kazi ikiwa katika upweke. Ufanisi wake hutegemea uhusiano imara kati ta taasisi za kisiasa na taratibu za kitamaduni. Hatua ya kwanza ya kutengana kwa muundo wowote wa mfumo wa uchaguzi unaotarajiwa huwa ni kuuliza: Muktadha wa kisiasa na kijamii ninaofanyia kazi ni upi? Swali la pili ni; Ninapanga mfumo wa kudumu au mmoja ambao unahitajika kutuwezesha kupitia kipindi cha mabadiliko?
Usipuuze Wapigaji Kura
Huku usahili ukiwa muhimu, ni hatari kutozingatia uwezo wa wapigaji kura wa kufahamu na kutumia kwa ufanisi aina mbalimbali za mifumo ya uchaguzi iliyo tofauti. Mifumo changamano inayopendelewa, kwa mfano, imetumiwa kwa ufanisi katika nchi zinazoendelea katika maeneo ya Asia-Pacific huku uzoefu wa uchaguzi mwingi wa hivi karibuni katika demokrasia mpya/changa umewekea viwango tofauti muhimu kati ya ukosefu wa elimu wa utendakazi na ukosefu wa elimu wa kisiasa. Hata katika nchi maskini zaidi wapigaji kura huwa, na hutaka kuelezewa, mipango yenye maendeleo makubwa ya upendeleo na uteuzi wa kisiasa. Kufanya majaribio na makundi yenye malengo fulani kwa ufanisi huweza kutoa habari muhimu kuhusu ni ipi itahitaji na ipi ambayo haihitajiki.
Fanya Makosa Upande wa kujumuishwa
Panapowezekana, iwe ni katika jamii zilizogawanywa an zenye kundi moja lenye sifa sawa, mfumo wa uchaguzi unastahili kuwa na makosa kwenye upande unaojumlisha mapendeleo muhimu bungeni. Bila kuzingatia ikiwa wachache wana mitazamo yenye utambuzi wa kiitikadi kikabila, kirangi, kilugha, kieneo au kidini, uondoaji wa aina muhimu za maoni kutoka kwa wana bunge, hasa katika nchi zinazoendelea umekuwa kwa kawaida na matokeo ambayo yana athari kubwa.
Mchakato ni Suala Muhimu Katika Uteuzi
Njia ambayo hutumiwa kuchagua mfumo fulani wa uchaguzi huwa pia ni muhimu katika kuhakikisha uhalali wake kwa jumla. Mchakato ambapo makundi mengi au yote hujumlishwa wakiwemo wapigaji kura kwa jumla huweza kusababisha makubaliano makubwa kuhusu matokeo ya mwisho kuliko uamuzi unaochukuliwa kuwa wenye msukumo wa chama fulani wa upendeleo wa kibinafsi pekee. Hata kama mahitaji yenye upendeleo fulani hukwepwa wakati wa kujadili uteuzi wa mifumo ya uchaguzi, ufuasi kutokana na vyama vingi na umma kwa taasisi yoyote ni muhimu ili iweze kukubaliwa na kuheshimiwa. Mabadiliko haya katika mfumo wa uchaguzi huko New Zealand kutoka mfumo wa FPTP hadi kwenye MMP, kwa mfano, yalihusu kura za maoni mara mbili ambazo zilitumiwa kuhalalisha matokeo ya mwisho. Kwa kulinganua, uamuzi wa serikali ya French Socialist mwaka wa 1986 wa kuhama kutoka kwa mfumo wa Awamu – mbili uliokuwepo hadi kwenye mfumo wa PR ulitazamwa na wengi kama wenye msukumo wa uzingatiaji wa upendeleo wa chama na ulibatilishwa kwa haraka punde tu serikali ilipopoteza uongozi mwaka wa 1988.
Hakikisha Uwepo wa Uhalali na Ukubalifu Miongoni mwa Washikadau Wote Muhimu
Makundi yote ambayo yangependa kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia yanastahili kuhisi kuwa mfumo wa uchaguzi utakaotumiwa ni wa haki na unawapatia nafasi sawa za ufanisi katika uchaguzi kama mwingine wowote. Lengo muhimu/kuu linastahili kuwa wale ambao hupoteza katika uchaguzi hawastahili kufasiri kutamauka kwao kuwa kutopendelewa kwa mfumo wenyewe au kutumia mfumo wa uchaguzi kama sababu ya kutatiza njia ya kuimarisha demokrasia. Katika mwaka wa 1990 huko Nicaragua, Sandinistas walichaguliwa na kutolewa kwenye serikali lakini wakakubali kushindwa shingo upande kwa sababu walikubali, usawa wa mfumo wa uchaguzi. Cambodia, Mozambique na Afrika Kusini waliweza kumaliza vita vya kikabila vilivyokuwa na umwagikaji wa damu kupitia mipango ya kitaasisi ambayo ilikubalika na wengi kutoka pande zote.
Jaribu Kuongeza Hadi Kileleni Athari/Matokeo ya Wapigaji Kura
Wapigaji kura wanastahili kuhisi kuwa uchaguzi huwatolea hatua zenye athari kwenye serikali na kwenye sera za serikali. Uteuzi huweza kufikishwa kwenye kilele kupitia njia mbalimbali. Wapigaji kura huweza kuchagua kati ya vyama, kati ya wagombeaji kutoka chama kimoja. Pia wanaweza kupiga kura chini ya mifumo tofauti wakati wa uchaguzi wa uraisi, chemba cha juu, chemba cha chini, kieneo na wa serikali za mitaa. Wanastahili kuamini kuwa kura zao zitakuwa na athari halali katika uundaji wa serikali sio tu katika muundo wa bunge.
Lakini Hakikisha Kuna Usawa Dhidi ya Kuvipa Moyo Vyama vya Kisiasa Vyenye Mshikamano
Tamaa ya kufikisha upeoni ufuasi wa wapigaji kura inahitaji kusawazishwa dhidi ya uhitaji wa kuvipa moyo vyama vya kisiasa ambavyo vina mshikamano na uwezo. Uteuzi wa juu wa mpigaji kura kwenye karatasi ya kura huweza kutoa bunge ambalo limetofautiana hivi kwamba hakuna yeyote atakayepata matokeo aliyoyatarajia. Huwa kuna makubaliano yaliyoeneo miongoni mwa wanasayansi wa kisiasa kwamba vyama vya kiasi vilivyoenea sana na vyenye muumano huwa miongoni mwa masuala muhimu katika kuinua kiwango cha demokrasia yenye ufanisi na ya muda mrefu.
Uthabiti wa Muda Mrefu na Faida ya Muda Mfupi Huwa Haviendani
Wakati ambapo wahusika wa kisiasa wanapojadiliana kuhusu mfumo mpya wa uchaguzi, kawaida huwa wanasukumiza mapendekezo ambayo wanaamini kuwa yatafaidi chama chao katika uchaguzi unaofuata. Hata hivyo huu unaweza kuwa mkakati potovu hasa katika nchi zinazoendelea kwa sababu ufanisi wa muda mfupi wa chama kimoja au kuvuma kwake huweza kusababisha kipindi kirefu cha uharibifu wa kisiasa na ukosefu wa utulivu wa umma. Kwa mfano wakati wa majadiliano kabla ya uchaguzi wa kuleta mabadiliko wa mwaka wa 1994, chama cha ANC cha Afrika Kusini wangedai kuendelea kutumia mfumo wa uchaguzi wa FPTP uliokuwa na ambao ungewapatia, kama chama chenye ufuasi mkubwa, kiti cha ziada zaidi ya mgao wake wa kura ya kitaifa. Ukweli kwamba walidai kuwepo kwa muundo wa PR na hivyo basi wakashinda viti vichache kuliko vile wangekuwa navyo chini ya mfumo wa FPTP, ulikuwa agano (testament) la hali ya kupata kipindi kirefu cha utulivu kama chenye kupendeza zaidi ikilinganishwa na kipindi kifupi cha utoshelevu wa uchaguzi. Hivyo basi mifumo ya uchaguzi huhitaji kuwa yenye kuwa tayari kutumika kwa ufanisi katika hali za kisiasa zinazobadilika na maendeleo ya mikondo mipya ya kisiasa. Hata katika demokrasia zinazoendelea, ufadhili wa vyama vikubwa huwa si tulivu, huku siasa katika demokrasia changa huwa imara na chama ambacho hufaidi kutokana na mpangilio wa uchaguzi katika uchaguzi mmoja huweza kukosa kufaidika katika uchaguzi wa pili.
Usifikirie Kwamba Mfumo wa Uchaguzi ni Suluhisho la Maovu Yote
Huku ukweli ukiwa kwamba mtu anapotaka kubadilisha hali ya ushindani wa kisiasa, mfumo wa uchaguzi huweza kuwa chombo muhimu zaidi cha kufanya hivyo, lakini mifumo ya uchaguzi haiwezi kuwa suluhisho la maovu yote ya kisiasa nchini. Matokeo ya jumla ya mambo mengine hasa utamaduni wa kisiasa wa nchi, huwa na athari zaidi kwenye matarajio yake ya kidemokrasia kuliko masuala ya kitaasisi kama vile mifumo ya uchaguzi. Zaidi ya hayo, athari changa za mfumo wa uchaguzi uliopangwa vizuri huweza kwa urahisi kuwa sehemu ya usambazaji (dispensation) usiofaa wa kikatiba, udhibiti wa nguvu za chuki za ndani kwa ndani au uzito wa tishio kutoka nje ya nchi kwenye utawala wa nchi.
Kwa Upande Mwingine Usipuuze Athari Zake
Ulimwenguni kote vikwazo vya kijamii kuhusu demokrasia huwa vingi, lakini bado vinaacha nafasi ya mkakati wa kisiasa wenye ufahamu ambao huweza kuendeleza au kutatiza ufanisi wa kidemokrasia. Uendeshaji wa uchaguzi wenye maarifa hauwezi kuzuia au kufutilia mbali uadui uliokita mizizi, lakini taasisi zinazofaa huweza kuashiria kwa kudukua mfumo wa kisiasa na kusababisha upungufu wa ugomvi na uwajibikaji mkubwa wa serikali. Kwa ufupi, huku mabadiliko mengi ambayo huweza kuafikiwa na mifumo ya uchaguzi iliyorekebishwa huwa kawaida pembeni. Kawaida athari hizi za pembeni ndizo huleta tofauti katika demokrasia inayowekwa pamoja au demokrasia inayopuuzwa.
Uwe Mwenye Kushughulikia (Mindful) Uwezo wa Kujitolea kwa Wapigaji Kura wa Kukubali Mabadiliko
Mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi huweza kuwa wazo zuri kwa wanasiasa wa ndani wanaoelewa udhaifu wa mifumo iliyoko, lakini ikiwa mapendekezo ya mabadiliko yanawasilishwa kwa njia inayofaa, wananchi/umma huweza kukataa kuvuruga (tinkering) mfumo, wakichukulia mfumo kama njia inayotumiwa na wanasiasa kubadilisha sheria ili ziwafaidi wenyewe. Hali zenye athari zaidi ni wakati mabadiliko huonekana kama ujanja ulio wazi wa kujifaidi kisiasa (kama ilivyokuwa huko Chile mwaka wa 1989), huko Jordan mwaka wa 1993 na huko Kyrgyzstan mara kadhaa tangu mwaka 1995, au wakati mfumo hubadilika kila wakati kiasi cha kwamba wapigaji kura hawajua waliko (kama jinsi baadhi ya watazamaji wanavyodai wa jinsi hali ilivyo huko Bolivia)
.
Na Usichukulie Kwamba Matatizo Huweza Kurekebishwa kwa Urahisi
Mifumo yote ya uchaguzi husababisha uwepo wa washindi na washindwa, hivyo basi masilahi yao. Hata hivyo, katika wakati wa mabadiliko inaweza kuwa si vizuri kuchukulia kuwa itakuwa rahisi kupata kukubalika baadaye ili kurekebisha matatizo ambayo huweza kutokea. Ikiwa marekebisho ya mfumo yanapangiwa, inaweza kuwa vizuri kuijumlisha kwenye chombo chake cha sheria chenye mabadiliko ya mfumo. Chukua muda wa kutosha ili kufanikiwa mara ya kwanza.
Epuka Kuwa Mtumwa wa Mifumo Iliyopita
Hata hivyo, kawaida mifumo ya uchaguzi ambayo haifai kwa mahitaji ya demokrasia mpya huwa imeridhiwa au kuchukuliwa kutokana na vipindi vya kikoloni bila kufikiria jinsi itakavyofanya kazi katika uhalisia mpya wa kisiasa. Karibu nchi zote ambazo zilitawaliwa na Waingereza huko Asia, Afrika na Pacific kwa mfano, walichukua mifumo ya FPTP. Katika nyingi ya demokrasia hizi mpya hasa zile ambazo zinakumbana na migawanyiko ya kikabila, mfumo huu ulionekana kuwa haufai kwa mahitaji yao. Vivyo hivyo, inadaiwa kuwa nchi nyingi zilizotawaliwa na Ufaransa huko Afrika Magharibi ambazo ziliendelea kutumia mfumo wa TRS (kama vile Mali) walikumbana na mtawanyiko (polarization) wa hatari kutokana na hayo; na watawala wengi wa kipindi cha baada ya ukomunisti huendelea kutumia utokeaji mdogo au mahitaji ya wengi yaliyoridhiwa kutokana na kipindi cha Soviet.
Tathmini Athari Zinazowezekana Kutokana na Mfumo Wowote Mpya Kuhusu Migogoro ya Kijamii
Kama ilivyotajwa hapo mwanzoni, mifumo ya uchaguzi huweza kuonekana sio tu kama mkakati wa kuchagua wanabunge na maraisi lakini pia kama chombo cha kusuluhisha migogoro katika jamii. Baadhi ya mifumo katika hali nyingine huwapatia moyo vyama ili kutoa maombi ya kijumla ili kusaidia waliokuwa nje ya msingi wa ufuasi wao. La kusikitisha ni kwamba, hali kama hizi ulimwenguni hivi sasa huwa za kawaida kiasi cha kwamba uwepo wa mifumo ya uchaguzi isiyofaa huwa na jukumu la kuzidisha mazoea hasi ambayo tayari yapo, kwa mfano, kwa kuvipatia ari vyama ili wachukulie uchaguzi kama ushindani wa matokeo yoyote na hivyo basi kukaa kwa njia ya uadili na ya kujitenga kwa watu walio nje ya kundi wanalonasibiana nalo. Wakati wa kupanga taasisi yoyote ya kisiasa cha muhimu ni kwamba, hata kama haisaidii katika kupunguza hali ya ukosefu wa utulivu katika jamii, kwa kiasi inastahili kufanya mambo yawe bora zaidi.
Jaribu na Ufikirie Kuhusu Hali ya Dharura Isiyo ya Kawaida au Isiyowezekana
Kawaida, mifumo ya uchaguzi hupangwa ili kuepuka makosa ya hapo awali, hasa ya hapo karibuni. Uangalifu unahitaji kuwepo katika kufanya haya ili kutochukua hatua na kuweka mfumo ambao unajitenga zaidi katika kurekebisha matatizo yaliyopo. Zaidi ya hayowapangaji wa mifumo ya uchaguzi watafanya vizuri ili kujiwekea maswali yasiyo ya kawaida ili kuepuka aibu wakati huo. Itakuwaje ikiwa hakutakuwa na mshindi chini ya mfumo uliopendekezwa? Inawezekana kwamba chama kimoja kinaweza kushinda viti vyote? Itakuwaje ikiwa utatuza viti zaidi ya nafasi zilizopo bungeni: Utafanyaje ikiwa wagombeaji watakuwa na idadi sawa ya kura? Mfumo unaweza kumaanisha, katika baadhi ya wilaya ni bora kwa mfuasi wa chama kukosa kupigia kura chama au mgombeaji wanayempenda?

