Katika mtazamo wa kiuchaguzi, ‘‘mfumo wa kisheria’’ una maana finyu na pana vilevile.
Katika mtazamo wa karatasi hii, ‘‘mfumo wa kisheria’’ unaeleweka katika maana hizo mbili.Tunaazimia kubuni maana ya ‘‘mfumo wa kisheria’’ kwa mapana ili tuweze kupata uelewa wa kina kuhusu maana ya kauli hiyo.
Mfumo wa kisheria ni fungu la kanuni za kisheria kuhusu haki za upigaji kura zinazotumiwa na wananchi ili kuwachagua maafisa wa kuwawakilisha. Hata hivyo, mfumo wa kisheria unaweza kufungamanishwa pia na kanuni za uchaguzi zinazowapa wananchi mamlaka kutumia uwezo wa umma kivyao (kwa kutumia vyombo vya kisheria ili kutimiza malengo ya kisheria, kueleza sera zinazohusu umma, kumwondoa ofisa yeyote wa umma).
Mfumo wowote wa kisheria, unaochukuliwa kama fungu la kanuni za kikatiba, kisheria, kiutawala na kiusimamizi, unaweza pia kuonekana kama mbinu iliyopo ya kiufundi inayolenga ya kuikuza ama demokrasia wakilishi au isiyo dhahiri.
Ni lazima itambuliwe kwamba uchaguzi si njia ya pekee ya kuwachagua maafisa wa umma (kuna teuzi za kisheria na zisizo kuwa na taratibu maalumu ; isitoshe, chaguzi pia huendeshwa na asasi za kivyuo kama vile bodi za mashirika zisizofuata sheria zozote zile za uchaguzi) wala kutumiwa katika kuwateua maafisa wa umma. Kwa yakini, wananchi pia hutumia uchaguzi kukubali au kukataa miswada ya kisheria, maamuzi ya serikali au maamuzi yanayochukuliwa na wasimamizi wa umma. (Kura ya maamuzi, kesi za pamoja mahakamani na kumng’atua mtu mamlakani hutumiwa kufanya hivyo).
Mada ya “mfumo wa kisheria’’ imefungamanishwa katika sehemu tatu kuu: masuala ya kutanguliza, vibadala vya kimsingi, na vipengee muhimu.
Kategoria ya kwanza imegawika katika sehemu tatu kuu.Ya kwanza inapendekeza maelezo ya kijumla ya uchaguzi, yanayohusisha kijelezi cha ‘‘mfumo wa kisheria’’, yaliyomo katika mada hiyo na mbinu inayofuatwa kuujenga. Ya pili, inayorejelea kanuni zinazotoa mwongozo, inatoa maelezo kwa ufupi kuhusu kanuni za kimataifa na kimaeneo zinazopatikana katika mikataba na makubaliano ambayo ni lazima yatiliwe maanani katika kuunda ama kurekebisha sheria za uchaguzi.Ya tatu imejikita katika uchanganuzi wa kihistoria na kisheria hasa katika yale masuala ambayo ni lazima yazingatiwe ili kuwezesha kuwepo kwa taratibu za kisheria. Ni muhimu kueleza kuwa, uchunguzi wa taratibu tofauti za kisheria hufanywa.
Sehemu ya viteuzi vya kimsingi, ambavyo ni lazima vizingatiwe ili kujenga mfumo wowote wa sheria, inaonyesha utafiti kuhusu mifumo ya kisiasa na himaya za kisiasa. Utafiti kama huo unaangazia njia tofauti tofauti za kupanga mamlaka ya umma kwa misingi ya mipaka na vilevile mbinu zinazoweza kuchukuliwa na serikali ya kidemokrasia kwa kurejelea ushindani wa kiuchaguzi wa vyama vya kisiasa. Inafafanua pia demokrasia wakilishi na zisizo dhahiri, vyombo vya kisheria vinavyounga mkono mifumo ya kisheria na michakato ya kubuni na kurekebisha vyombo kama hivyo.
Kategoria ya tatu inachunguza vipengee muhimu vya mifumo ya kisheria. Mada tofauti tofauti zinachunguzwa hapa ifuatavyo: mifumo ya uchaguzi, usimamizi wa uchaguzi, kuweka mipaka ya wilaya, sajili ya wapigakura, mafunzo ya wapigakura, wagombea na vyama vya siasa, uendeshaji wa uchaguzi, kuhesabiwa kwa kura, uhusiano kati ya uchaguzi na teknolojia na uadilifu wa uchaguzi.Vilevile, utafiti wa kina kuhusu mbinu tofauti za kutatua mizozo inayotokana na uchaguzi hufanywa na uainishaji kufanywa kutokana nao. Nafasi inayochukuliwa na usimamizi wa uchaguzi wowote ule katika mgao kama huo hutegemea nafasi zinazochukuliwa na simamizi hizo katika mataifa yao. Uchunguzi linganishi kuhusu mifumo ya kukata rufaa katika mizozo kuhusu uchaguzi pia hufanywa, na hujumuisha maelezo kuhusu makataa, kanuni kuhusu ushahidi na kufutiliwa mbali kwa uchaguzi.
Sura ya mwisho inanuia kukusanya taarifa yote katika maelezo ya mwisho. Hapa, mazingatio kuhusu gharama ya huduma hii hupatikana kutokana na chunguzi zote.
Sehemu nzima ya Mada ya ‘‘Mifumo ya Kisheria’’ hunuia kuboresha taarifa iliyoko, na kuiongezea jambo lolote muhimu na kuifanya kuwa pana na ya kueleweka.
Hivyo basi, mada hii hudai kudokeza jinsi wajibu wa kiuchaguzi unaotekelezwa na mfumo wa kisheria unavyoweza kuwa.
Mbinu dhahiri hutumiwa ili kumsaidia msomaji kupata picha ya wazi ya mada kabla masahihisho yoyote yafanywe kuhusu yaliyomo.Wasomaji hunufaishwa kwa sababu wao hufikishwa kwenye mada kuu za kijitabu hicho wakiwa na ufahamu mzuri kuzihusu. Sehemu fulani huundwa ili kuweka wazi miktadha ambamo chaguzi na mifumo ya kisheria zimejikita.
Masuala muhimu kabisa hupatikana katika sehemu mbili, ambazo pia zinajumuisha mada nyingine nyingi zinazohusiana na mada kumi na moja za mradi wa ACE.
Sehemu ya kwanza inanuia kuchunguza njia mbadala za kimsingi ambamo uchaguzi unaweza kuendeshwa. Hapo, uwezekano wa aina tatu unachanganuliwa: kesi za Demokrasia dhahiri na isiyo dhahiri, kuwepo kwa mbinu za kisheria na njia zinazofuatwa ili kuzua na kurekebisha mbinu za kisheria. Sehemu hii huonyesha mambo yote ya kuchaguliwa yaliyoko katika kutoa kielelezo, kurekebisha na kuweka katika hati za kisheria mfumo wa uchaguzi.
Sehemu ya pili kwa upande wake inahusu vipengee muhimu vya taratibu za kisheria. Utafiti huu huchanganua mada tofauti ambazo ni pamoja na mfumo wa uchaguzi, uhusiano kati ya uchaguzi na teknolojia, usimamizi wa uchaguzi, kutatuliwa kwa mizozo ya uchaguzi na matini ya mwisho ambayo imetathmini matokeo yote yanayowezekana.