Uainishaji wa kisasa wa aina za serikali hutofautisha kimsingi kategoria mbili: Mfumo wa bunge ya Ulaya na wa Urais wa Marekani. Kutokana na mpangilio wa kila moja ya mamlaka ya serikali, mahusiano kati yao na njia ambayo zinahusiana, kimsingi, tawi la uamuzi na la kisheria, zinaweza kutambulisha kati ya mfumo mmoja na mwingine.
Mfumo wa kirais unatokea katika katiba ya Marekani na inatambulika kwa: a) mamlaka ya rais ni ya umoja yaani yanafungamanisha mkuu wa serikali na kiongozi wa nchi; b) rais huchaguliwa na watu na si kwa mamlaka ya kisheria ambayo humpa uhuru mwingi kuhusiana na ya awali; c) rais huwateua na kuwaondoa watu wa kuhudumu katika baraza la mawaziri, mawaziri na makarani wa serikali aamuavyo; d) Rais, makarani wa serikali na mawaziri hawawajibiki kwa baraza; e) rais, mawaziri, makarani wa serikali na wadau katika baraza la umma hawawezi kuwa wanachama wa baraza; f) Rais hawezi kuwa mwanachama wa chama tofauti na kile kilicho na wawakilishi wengi katika baraza; na g) rais hawezi kuvunja baraza wala baraza kupitisha kura ya kutokuwa na imani kwa rais.
Mfumo wa bunge unatokana na mabadiliko ya kisiasa ya nchi nyingi za Ulaya hasa Uingereza na ina sifa zifuatazo: a) wanachama wa baraza la mawaziri (mamlaka ya uamuzi na serikali) ni wanachama wa bunge pia; b)baraza la mawaziri linajumuisha viongozi wa vyama ambavyo kwa pamoja vimetoa wawakilishi wengi bungeni; c) mamlaka ya uamuzi yamegawanywa kati ya kiongozi wa nchi mwenye uwakilishi katika vikao vya hadhi na mkuu wa serikali anayeshughulikia utawala na serikali yenyewe; d)Katika baraza la mawaziri pana mtu anaye julikana kama waziri mkuu mwenye mamlaka mengi ya kisiasa katika serikali; e) baraza la mawaziri huweza kujikimu kwa kuungwa na wengi kati ya walio bungeni; f) utawala wa umma ni jukumu la baraza la mawaziri chini ya uangalizi wa mara kwa mara wa bunge ambao wanaweza kushurutisha serikali kuwajibika; g) kuna utawala wa kwa pamoja kila mara kati ya serikali na bunge; h) bunge inaweza kukataa kura ya imani ama hoja ya lawama kwa baraza la mawaziri ambapo watalazimika kujiuzulu, serikali inaweza kumwomba kiongozi wa nchi avunje bunge.
Isitoshe, aina nyingine ya serikali inaweza kuelezwa: serikali ya mabavu ni ile ambayo kiongozi ama dikteta hutumia mamlaka yake atakavyo. Hali kama hii hutokea pale ambapo upeo wa mgogoro hutukia na inaaminika na wengi kuwa serikali haiwezi kutatua suala lililopo. Vilevile inaweza kuwa imetokana na kura ya maoni ama makundi ya watu waliojihami ama mageuzi ya serikali.Wa kwanza huunda serikali yenye viongozi wenye haiba kubwa wa mwisho huunda serikali za kimabavu ama kidikteta. Serikali hii ya kimabavu hujaribu kuimarisha wanaoiunga mkono kwa kuingilia maisha ya jamii kwa kiwango kikubwa kwa kuanzisha chama kisicho na kifani na propaganda ama kwa kutumia jeshi. Udikteta unaweza kuzua serikali ya kiimla.
Ni muhimu kutafiti aina ya serikali (ya kirais, kibunge ama ya kimabavu) ili tuweze kujua uwezekano wa kuwepo kwa asasi na umbo la kisheria la shughuli za uchaguzi. Hii kwa minajili ya uwakilishi na utenda kazi umehakikishwa katika mfumo wa uchaguzi, pamoja na utawala wa ule wa kisiasa. Bila shaka, ni wazo zuri kurejelea masuala ya kiufundi ya kimuktadha ya kitamaduni, kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa kurejelea mifumo ya kiserikali na kibunge.