Kanuni za utawala zinazotolewa na mamlaka ya uchaguzili kudhibiti masuala
mahsusi ya kiutawala kwa njia sahili. Kanuni kama hizi ni legevu hivyo basi
zinaweza kubadilishwa kwa urahisi kuliko taratibu za kisheria.
Wakati wa uchaguzi, masuala ya utawala yanapaswa kutatuliwa kwa dharura na
kwa haraka.
Sheria za uchaguzi hazilazimiki kudhibiti masuala kama hayo na yanaweza
kubadilika uchaguzi baada ya mwingine.
Kanuni za kiutawala husaidiana na sheria za uchaguzi, na ni lazima zitolewe
na halmashauri ya kusimamia uchaguzi iliyo na jukumu la kuendesha uchaguzi
kutoka kwa mtazamo wa kisheria. Halmashauri za kusimamia uchaguzi zilizo na
uwezo wa kusimamia hatua za uchaguzi lazima zirekebishe marekebisho ya kawaida
au ya kikanuni. Kuna miundo tofauti ya uchaguzi yenye mamlaka ya kufanya kazi
kama hii. Kwa kawaida, mashirika haya huwa yasiyobadilika na ya muda.
Katika nchi zenye halmashauri huru za kusimamia uchaguzi, halmashauri hizo
zina uwezo wa kutoa kanuni za utawala. Azma ya nchi ni kukataza kuwepo kwa
kanuni zisizotekeleza kanuni za utawala kuruhusu mamlaka ya uchaguzi kusimamia
masuala mahsusi kama jinsi vyama vya kisiasa vinaandikisha ripoti zao na jinsi
ya kushughulika usajili wa wagombeaji, kampeni za uchaguzi, matangazo ya
uchaguzi, siku ya uchaguzi na kadhalika.