Vigezo vya kisheria ni muhimu katika kufungamanishwa kwa mfumo wa uchaguzi
wa kisheria. Madai haya yanarejelea mabadiliko ya muhimu sana: mizozo ya
kiuchaguzi hayatatuliwi tu na mamlaka ya kisiasa pekee lakini pia na mya
kisheria (kwa upande mmoja kuna kesi ambazo kuamuliwa kwa mzozo wa uchaguzi
hufanywa na korti na kwa upande mwingine kesi nyingine zinaweza kuonekana kama
zinazohusisha mifumo ya mseto ambapo mamlaka ya kisheria na kisiasa yana jukumu
katika kutatua mizozo ya uchaguzi) mamlaka ya kisiasa hutumiwa kutatua mizozo
ya uchaguzi kwa kutumia mbinu za kisiasa. Sasa mizozo ya kisiasa inatatuliwa na
korti maalum za uchaguzi ambazo hutatua mizozo kwa kutumia mbinu za kisheria).
Kesi za uchaguzi zimewekwa katika sheria na maamuzi kutolewa na korti za
uchaguzi na majaji wa uchaguzi (zinazoweza kuchukuliwa kama vigezo vya
kisheria) na zimekuwa za kimsingi kuelewa jinsi sheria ya uchaguzi inapaswa
kuwa.
Katika mifumo ya kisheria, vigezo vya kisheria vinaweza kuchukuliwa kama
chanzo cha sheria (kinyume na hayo, mfumo wa sheria za kiraia, sheria
zinazowekwa huonekana kama chanzo cha sheria) kulingana na dhana za kisheria
kama stare decisis ama ratio decidendi sababu za kuunga maamuzi ya awali lazima
zitiliwe maanani ili kutatua kesi mpya na zinazolingana.Sheria za uchaguzi
hazielezwi kwa kanuni na sheria lakini kwa mitazamo ya kimahakama.
Katika mifumo ya sheria, korti za uchaguzi ni muhimu. Korti hizi huleta
mchango muhimu katika kuunda mfumo wa kisheria. Mitazamo ya mahakama
(inayotazamwa kama vigezo vya kisheria) huzua sheria, mitazamo ya kimahakama ya
uchaguzi (hutazamwa kama vigezo) huibua sheria za uchaguzi.
Mfumo unaojulikana kama wa Waingereza ama mfumo wa kesi za kawaida huwapa
majaji wa tawi la serikali la kisheria mamlaka ya kutatua mizozo ya uchaguzi
kikamilifu. Maamuzi yao kamilifu yana uwezo wa kukomesha mifumo changamano ya
kukata rufaa kesi za uchaguzi (ambazo zinaweza kuwa za kiutawala au kisiasa
kama tulivyoelezea awali).
Ni bayana kuwa kwa mifumo isiyo ya sheria za usawa (zinazojulikana kama
mifumo ya sheria za kiraia) maamuzi ya kisheria ya mizozo ya kiuchaguzi ni
muhimu. Majaji wa uchaguzi katika kesi za mfumo wa kiraia wametoa mchango
muhimu, ambao umeimarisha na kuleta maendeleo kwa sheria za uchaguzi. Katika
nchi hizo, vigezo vya kisheria vinatolewa na korti za uchaguzi na hutumiwa
kutatua kesi mpya.
Hukumu za mahakama za mizozo ya uchaguzi ni muhimu kiasi cha kwamba wakati
mwingine pia huamua iwapo amri zilizotolewa na mamlaka ya uchaguzi ni za
kikatiba. Hukumu za uchaguzi zinapofanya hivi zinaweza kutazamwa kama korti za
kikatiba zinazoleta ufafanuzi wa kikatiba.
Walioidhinishwa kutoa vigezo vya kisheria vya lazima ni mahakama za kitengo
cha juu.Vitengo hivi hutolewa kufuatia matakwa rasmi kutekelezwa kwa maamuzi
yaliyokubaliwa na wote ama yayotolewa. Vigezo vya kisheria (maarufu kama
utekelezaji wa sheria) huwekwa kwa kupia marudio ya matumizi ya mojawapo ya
ratio decidendi kutatua kesi zaidi ya moja. Kesi kama hizi lazima ziwe
zinalingana ili kutatuliwa kwa kutumia uwiano mmoja. Maamuzi ya mahakama za juu
kwa upande mwingine, mitazamo ya kisheria ambayo imefuatwa na korti tofauti pia
ni ya muhimu katika kuweka vigezo vya kimahakama. Kwa kawaida vigezo vya
kisheria vinaweza kukatizwa ama kuondolewa kwa uamuzi wa majaji wa vitengo vya
juu.
Vigezo vya kisheria na mitazamo ya kisheria huenea kufikia wapi? Athari zao
ni zipi? Ni watu wepi waliofungwa nazo? Ni mifumo ya kisheria iliyodhibitiwa
katika mitazamo ya kisheria na maamuzi ya kimahakama na yana jukumu la kutatua
masuala yanayopingwa katika kila kesi na ambayo ni ya lazima kwa korti na
majaji. Licha ya hayo, kuna mifumo ya kisheria ambayo mitazamo ya kimahakama na
vigezo vya kisheria vina athari ya kijumla (erga omnes) na mamlaka yanayoenea
yanayoathiri mamlaka yote na kubatilisha sheria zilizowekwa.