Mikataba yote inapaswa kuangaliwa kwa makini. Hili ni kweli hasa pale ambapo mazingatio ya ubora, bei na wakati ni muhimu. Waelimishaji wanapaswa kufikiria kuhusu jinsi watakavyozisimamia, na hawana budi kulipa hili wakati na kulitia maanani.
Waelimishaji Wanatofautishwa na Watoa huduma
Punde mkataba ukishatayarishwa, maswala ya usimamizi wa mradi huo yanaweza kutenganishwa na usimamizi wa mpango mzima wa elimu. Anayepewa kandarasi hiyo anaweza kufanya sehemu Fulani ya usimamizi (au yote) au kitengo Fulani cha usimamizi katika mpangilio wa waelimishaji au halmashauri ya kusimamia uchaguzi ichukue kandarasi hiyo.
Kwa hivyo uhusiano na mpango wa elimu unaweza kudhoofika, na inaweza kufanyika kuwa wale walioidhinisha kufanywa kwa kazi hiyo wanakoma kuitathmini na kuisimamia kwa karibu.
Ikiwa uwezo wa kielimu ni finyu, pana uwezekano kwamba aliyepewa kandarasi hiyo atachukua jukumu kubwa kwa mradi huo.
Athari ya hii ni kwamba habari zote zilizopo kuuhusu mradi huo, tathmini zake zote na mtindo wa utekelezaji wake hutoa uzingatifu mkubwa kwa anayepewa kandarasi, anayelipia gharama, anayeuza huduma hizo, anayezileta bili. Hii inaweza kuchukuliwa kama idhini ya kuchapisha pesa.
Uwezo wa Kusimamia mradi
Timu ya kuelimisha, au halmashauri ya kusimamia uchaguzi, ambayo huagizia bidhaa na huduma, iwe kwa kiwango kikubwa au kiwango finyu, inapaswa kuhakikisha kwamba ina uwezo wa kusimamia kandarasi zote kwa kina. Ujuzi wa kusimamia mradi, mikutano ya mara kwa mara, marekebisho ya malengo na gharama, na mazingatio ya tofauti katika gharama, ubora wa huduma zinazotolewa, na maelezo ya kina kuuhusu mradi huo vinapaswa kuzingatiwa pamoja na anayepewa kandarasi na mtoaji wa huduma hizo.
Hili kwa kiasi Fulani ni suala la uaminifu, na kunaweza kuwa na kauli kwamba watoa huduma waaminifu wanaofanya kazi kwa makubaliano Fulani wanaweza kuusimamia wenyewe. Hata hivyo pia ni suala la ufahamu na uwezo.
Watoa huduma wakiachiwa kufanya shughuli hizo wenyewe, wanaotekeleza mradi huo bila kuangaliwa, wanaweza kuibukia kuwa wajuzi. Ya kwanza ni tatizo la kandarasi za siku za baadaye – mjuzi ana nafasi kubwa kuhusiana na miradi ya siku za usoni na anaweza kuweka bei ikiwa hapana njia mbadala ya kuhakikisha kazi hiyo inafanywa. Tatizo la pili ni kuhusu uwezo wa wafanyakazi – mtoa huduma aliye na ujuzi halinganishwi na mpewa kandarasi aliye na ufahamu mkubwa kuhusiana na mradi huo, hivyo basi wanakuwa na uwezo kutumia mamlaka yao.
Huduma katika Kipindi Kifupi
Nyenzo za kusimamia mradi, katika kipindi kifupi, zinaweza kushughulikiwa kwa kuzitafutia huduma hizo kivyake tofauti na bidhaa na huduma zinazochukuliwa ili kusanifu bidhaa na huduma za shughuli hiyo. Hili mara nyingi hufanywa na halmashauri na mashirika mapya ya kusimamia uchaguzi. Hata hivyo, wale wanaonuia kutumia bidhaa na huduma hizi kila mara wanapaswa kuukuza uwezo huo katika wafanyakazi wake.
Uwezo wa wafanyakazi wenyewe unaweza kujengwa katika kandarasi, hivyo basi timu ya kusimamia mradi huo inapaswa kuuacha ujuzi huo katika ofisi hizo kwa kuwafundisha na kuwasaidia wafanyakazi wa mifumo asilia ya maeneo hayo.