Orodha ya Elimu kwa Raia na Wapigakura
Uhusiano kati ya elimu na maisha ya raia uliwekwa na Aristotle:
“Hata hivyo bora zaidi katika njia hizo zote … ili kulinda uthabiti wa katiba … ni mfumo wa elimu unaozingatia Katiba hizo”(Siasa V vii 20).
Sehemu hiyo ya mada inachukulia kuwa shughuli ya kielimu inatarajiwa kuhimiza na kuendeleza demokrasia. Inawezekana vizuri kabisa kuwazia mradi wa elimu kwa raia ambao unatarajiwa tu kuendeleza uraia uliokuzwa katika nchi iliyoendelea lakini ambayo kimsingi ingali inashikilia uongozi wa kikabila- mazingira ambao istilahi hii iliibuka, kwanza katika Urumi na kisha katika maeneo ya mijini wakati wa Malkia Elizabeth wa kwanza wa Uingereza.
Huu ni utangulizi kuhusu elimu kwa raia na elimu kwa Wapigakura, sehemu muhimu lakini ndogo ya elimu kwa raia. Inatalii uwezekano na vikwazo au matatizo katika elimu kwa umma kama njia ya kuafikia demokrasia katika mazingira tofauti ya kisiasa. Itafafanua baadhi ya istilahi zinazotumika ulimwenguni na mazingira ya kitaasisi ambazo ni bora zaidi, na kisha itatoa vifaa kamilifu na ratiba ya utekelezaji kwa mtu anayetoa elimu kwa raia. Mwongozo unatolewa kuhusu mbinu mbalimbali, njia na nyenzo, na sehemu zinazohusiana na ugharamiaji, usimamizi, utathmini, ukadiriaji na urasmishaji au uanzishaji wa taratibu.
Eneo la mada linazingatia elimu kwa raia na kasha, panapofaa, taratibu mahususi za elimu kwa Wapigakura ambazo ni muhimu katika maandalizi ya uchaguzi. Taasisi zenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi ambazo zina wajibu mkubwa kwa raia zitapata haya yakiwa yamejadiliwa pamoja na jukumu mahususi la elimu kwa Wapigakura au hata wajibu wa kutoa habari kwa Wapigakura ambalo mashirika mengine yanayosimamia uchaguzi yanalazimika kutekeleza. Sehemu kubwa ya matini hii inahusu elimu kwa ujumla, isipokuwa pale inaporejelea jukumu linalotegemezwa katika utoaji wa elimu kwa umma.