Kuna aina tatu za kijumla za usajili wa wapigakura:
- orodha ya muda
- rejista au orodha endelevu
- rejista ya raia
Kila mojawazo ina ubora na udhaifu wake, na hakuna yoyote iliyo bora kwa nchi au hali zote. Ni muhimu kuteua mfumo utakaoafiki mazingira ambamo mfumo huo utatumika.
Orodha ya muda ndiyo nyepesi mara nyingi. Orodha mpya ya wapigakura stahifu kutengenezwa kwa kila tukio la uchaguzi na hakuna haja ya kuitunza kama yenye usasa, ulinagnifu au kamilifu baada ya tukio hilo. Kwa hivyo, orodha ya muda huhitaji usaidizi mdogo wa kiusimamizi kati ya chaguzi. Hata hivyo, kuunda orodha hii kunataka juhudi kubwa kutoka kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi katika kipindi cha kukaribia uchaguzi, aghalabu kwa kutumia wafanyakazi wa muda.
Rejista au orodha endelevu hujengeka kutokana na juhudi za kabla za usajili, na nia ya kila mara kuwa na orodha ilyosasaishwa. Hili hutaka juhudi muhimu za usimamizi uliopo. Tokeo huwa kwamba halmashauri ya kusimamia uchaguzi itahitaji wafanyakazi wengi wakati wote wa maisha ya uchaguzi (yaani, kipindi kizima cha kutoka kwenye uchaguzi hadi mwingine). Kuweka usasa katika orodha huchochea kuchunguza mabadiliko katika watu: raia waliofikisha umri wa kupiga kura; vifo; watu waliopoteza haki ya kupiga kura kwa sababu ya kushtakiwa kwa makosa ya jinai; au kubadilisha anwani. Maeneo mengi mahitaji rasmi au ya kisheria kwa raia kutoa taarifa kwa halmashauri ya kusimamia kuhusu mabadiliko katika hali zao katika wakati maalumu. Ili kupata taarifa hiyo inayohitajika katika kusasaisha rekodi katika orodha endelevu, halmashauri hutaka mwafaka wa kuongoza utumizi deta kwa ushirikiano na wizara nyingine za serikali au mashirika ya umma kama vile ya kutoa leseni za madereva (sajili za magari), idara za kutoza ushuru na posta. Masahihisho kupitia kwa utumizi deta kwa ushirikiano hurahisishwa ikiwa kila raia anapewa na kutumia nambari ya kitambulisho; bila hilo inaweza kuwa vigumu kulinganisha faili.
Juhudi kubwa zaidi za kiusimamizi zinahitajika katika sajili ya raia. Hii ni rejista ya watu inayojumuisha jina na sifa nyingine tambulishi za raia kama vile nambari ya kitambulisho, siku ya kuzaliwa, anwani na jinsia. Hutumiwa kwa majukumu mbalimbali ya umma. Moja katika haya ni kutengeneza orodha ya wapigakura itakayotumiwa kwa uchaguzi. Sajili ya raia hutunzwa halmashauri nyingine kando na halmashauri za uchaguzi – pengine idara ya utozaji ushuru. Wananchi wanapaswa kusasaisha taarifa katika sajili ili kuendelea kupokea faida mbalimbali za kijamii, vikiwemo elimu, matibabu na faida za ufanyakazi. Halmashauri ya kusimamia uchaguzi huwa na wajibu mdogo katika kusasaisha orodha ya wapigakura, kwa wepesi kupokea taarifa hii kutoka kwa sajili ya raia. Hili huipa halmashauri ya kusimamia uchaguzi jukumu dogo na udhibiti mdogo sana kwenye ubora wa orodha hiyo kuliko ambavyo ingekuwa nalo ikiwa rejista hiyo endelevu ingetunzwa.
Orodha ya Muda