Orodha Endelevu – Faida / Uzuri —
Skip to content.
|
Skip to navigation
Search Site
Advanced Search…
English
Español
العربية
Français
Swahili
Home
Encyclopaedia
Comparative Data
Electoral Materials
Support and Advice
Regions & Countries
About ACE
Personal tools
Log in
Practitioners' Network
You are here:
Home
→
Encyclopaedia
→
Mada
→
Usajili wa Wapigakura
→
Mambo ya Kijumla
→
Rejista Endelevu
→
Orodha Endelevu – Faida / Uzuri
face
Practitioner Login
English
Encyclopaedia
Info
Voter Registration
Topic Index
Orodha Endelevu – Faida / Uzuri
Orodha endelevu ina uzuri kadhaa:
Orodha ya wapigakura inafanywa kuwa ya kisasa kwa sababu inasasaishwa kila mara.
Orodha hiyo inaweza kuwa huru kukaguliwa na raia wakati wowote wa mwaka bali sio katika kipindi maalumu tu.
Kwa kuwa orodha hiyo huwa tayari kila wakati, hakuna tatizo lolote hasa katika wakati wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu au mdogo (k.v. uchaguzi mdogo ili kujaza nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi).
Orodha ya mwisho ya wapigakura inaweza kutayarishwa upesi. Mara nyingi huwa kuna kipindi cha kusahihisha orodha wakati wa kampeni za uchaguzi ili kuhakikisha kwamba kila mtu anayestahili kupiga kura anapata fursa ya kujumuishwa kwenye orodha ya wapigakura. Kwa orodha ya muda, muda wa kampeni unaweza kutumiwa katika kutengeneza orodha asilia ya ya wapigakura pamoja na kusahihisha na hatimaye kutoa orodha ya mwisho. Kukiwa na orodha endelevu, orodha asilia huchukuliwa kuwa orodha iliyopo mwanzoni mwa kampeni za uchaguzi. Kwa sababu hii, kipindi rasmi cha uchaguzi kinaweza kufupishwa kwa muda ambao ungetumika kutengeneza orodha asilia ya wapigakura.
Mabadiliko na masahihisho yanaweza kufanywa katika mwaka mzima na sio tu wakati wa harakati za uchaguzi. Hili hupunguza shinikizo la wakati na linaweza kutarajiwa kuimarisha ulinganifu wa orodha endelevu.
Matumizi ya orodha endelevu sio kwamba ni mfumo wa usajili wa wapigakura usiogharimu pesa nyingi. Hata hivyo, hutoa nafasis nzuri ya kuboresha ujenzi wa orodha ya awapigakura – kwa mfano, kupitia kwa utumizi deta kwa ushirikiano.
Orodha endelevu inaweza kutumiwa kwa kazi nyingine kama vile chaguzi za viwanda kule Australia, uundaji wa mabaraza Marekani au kuelekeza katika utengaji wa maeneo ya upigaji kura.
Katika orodha endelevu, viwango vya usajili wa wapigakura vinaweza kuwa zaidi kwa sababu usajili hufanywa kila mara. Kwa upande mwingine, maeneo mengi ymepata kwamba orodha endelevu si kamilifu tena kushinda orodha zilizojengwa kwa njia ya hesabu na huenda ukamilifu wake ukawa kwa kiwango cha chini kabisa.
Kuhusu kigezo cha usasa, utendakazi hutofautiana kutegemea aina ambalimbali za rejista endelevu. Wale wanaotaka kusasaisha taarifa kuwahusu wapigakura wanaweza kufanya kwa karibu karibu wanaweza kutarajiwa kuwa na usasa kila wakati. Zingatia kwamba kipindi cha masahihisho kina athari kubwa kwenye usasa. Ikiwa wapigakura wanaweza kusajiliwa siku ya uchaguzi, ni ama orodha ya muda au rejista endelevu inaweza kuwa na kiwango cha juu cha usasa kwa kuwa wapigakura wanapata nafasi ya kuripoti mabadiliko yoyote mapya wenyewe vituoni.
Katika mifumo ya majimbo, orodha endelevu huruhusu viwango mbalimbali vya serikali kugawana deta hivyo basi kupunguza uwezekano wa kunukuu. Hata hivyo, viwango mbalimbali vya mfumo wa majimbo vinaweza kutumia mbinu tofauti tofauti za kusajili wapigakura. Kwa mfano, katika kiwango cha majimbo Kanada huitunza orodha endelevu lakini baadhi ya mokoa yake hutumia orodha za muda.
Gharama ya kusajili wapigakura wapigakura husambazwa katika kipindi kizima kutoka kwa uchaguzi mmoja hadi mwingine hivyo basi kutoa nafasi ya kupanga bejeti ya kufaa. Hata hivyo bado huenda kukawa na gharama ya ziada wakati wa uchaguzi au katika shughuli ya usajili.
Kwa kuwa kazi huendelezwa katika muhula mzima wa uchaguzi, haja za ufadhili haziongezeki kivyovyote katika mwaka fulani au wakati maalumu.
Usajili wa Wapigakura
Contributors to Voter Registration
Bibliography
Contact
Privacy Policy
Terms of Use
Accessibility
Site Map
Copyright and Disclaimer
©
1998-2025 ACE project