Utambulisho wa wapigakura ni mchakato wa kukagua ustahifu wa wapigakura watarajiwa na kuingiza majina yao na taarifa nyingine za utambulisho kwenye orodha ya wapigakura. Mchakato huo unapaswa kuwa huru, pana na unaoshirikisha wote. Huu unataka mikakati kabambe ya kuhakikisha kwamba wapigwakura watarajiwa wanafahamu kuhusu mchakato huo wa uchaguzi na wana nafasi ya kutosha ya kuukamilisha. Mkakati mmoja kama huo ni kampeni ya elimu kwa wapigakura. Elimu kwa wapigakura husisitiza umuhimu wa usajili, kueleza majukumu ya wapigakura na kutoa taarifa kuhusu jinsi ya kujisajili.
Ni nani mwenye Jukumu – Raia au Serikali?
Mifumo tofauti tofauti inaweza kutumia mbinu tofauti tofauti za usajili na kugawa majukumu mbalimbali kwa wasimamizi wa uchaguzi na raia. Wakati mwingine usajili kimsingi ni jukumu la raia ambao ndio huanzisha mchakato kwa kuwasiliana na usimamizi wa uchaguzi. Kwa mfano, wanaweza kulazimika kujaza fomu ya usajili wa wapigakura katika kituo cha upigaji kura, kujaza fomu iliyotolewa kwenye wavuti wa tovuti ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi, au (katika nchi inayotumia sajili ya raia) kujaza mabadiliko katika fomu ya usajili na kuiwasilisha kwa halmashauri ya kushughulikia raia. Katika visa vingine, maofisa wana jukumu la kuwasiliana na wapigakura watarajiwa; mara nyingi wao hukusanya taarifa kuhusu usajili kwa kutumia wasajili wanaotembelea makazi ya wapigakura ama katika maeneo yote au lengwa. Hata hivyo, bado mbinu nyingine itakayotumiwa itategemea utumizi deta kwa ushirikiano kati ya halmashauri ya uchaguzi na mashirika mengine yanayoshughulikia raia kama vile posta au halmashauri ya kusimamia makao. Halmashauri ya kusimamia uchaguzi ikiarifiwa kuhusu mabadiliko kwenye taarifa kumhusu raia, inaweza kumtumia mpigakura nyenzo za usajili wa wapigakura kwa mtu huyo ili kuthibitisha mabadiliko hayo.
Kwa kawaida, raia na serikali mara nyingi hushirikiana katika jukumu la kuanzisha mawasiliano. Katika Mexico kwa mfano, ambyo hutumia orodha endelevu ya wapigakura, halmashauri ya kusimamia uchaguzi huwezesha usajili kwa kuweka vituo maelfu ya vituo vya usajili wa wapigakura vikiwemo vile vya kuhamishwa. Hata hivyo, bado ni jukumu la raia kuzuru maeneo ya usajili na kuanzisha rasmi mchakato huo wa uchaguzi.
Wapigakura wakianzisha mchakato huo, tajriba imeonyesha kwamba kuwa kwao katika nafasi nzuri ya kufanya hivyo kunaweza kuongeza pakubwa kushiriki kwao. Katika uchunguzi wa mwisho, ni suala la uwezo wa kufikia shughuli hiyo: je, serikali ina jukumu kiasi gani katika kuhakikisha kwamba raia wanajisajili bila tatizo lolote? Jibu litakuwa kwamba serikali inapaswa kuchukua kwa ukamilifu jukumu la kuhakikisha kwamba usajili hauwi kizuizi dhidi ya raia kushiriki katika chaguzi za kidemokrasia. Kwa wakati huo, gharama huwa jambo la muhimu katika kuamua viwango vya juhudi za kutumiwa katika usajili wa wapigakura.
Gharama na Ujumlishi - Mikinzano
Waundaji sera hung’ang’ana kupata ujumuishi katika mchakato wa usajili wa wapigakura japo ni lazima wapime juhudi zao dhidi ya gharama ya zoezi hilo zima. Kujenga orodha ya wapigakura huelekea kuwa nafuu ikiwa majukumu mengi ya usajili huo yanakuwa mikononi mwa wapigakura. Katika visa kama hivi, wajibu wa wasimamizi wa uchaguzi utakuwa kuhakikisha kwamba wapigakura wanafahamu kuhusu mahitaji na shughuli zinazoambatana na usajili wanazopaswa kuzingatia ili kujisajili. Wasimamizi hao wanaweza kuamua kutopuuza jukumu la kutambua wapigakura watarajiwa ambao watakosa kujisajili.
Mwelekeo huu huishia katika orodha za wapigakura ambazo zinaelekea kuwa jumuishi kuliko zile zilizotayarishwa kwamwanzo wa hatua za serikali. Isitoshe, makundi mengine ya raia mara nyingi huenda yakakosa kujitambulisha kama wapigakura stahifu na kujisajili. Mifano ni kama vile vijana, wazee na wasiojiweza, maskini na watu wasio na uwezo wa kusoma na kuandika, na wakazi wa maeneo ya mashambani ambako uchukuzi ni shida.
Mpigakura kuthibitisha Utambulisho wake