Usajili wa kujianzishia mwenyewe
Sawa na usajili wa kujitolea, usajili wa kujianzishi mwenyewe hutokana na mtazamo kwamba upigaji kura ni haki ya raia. Kwa sababu hii, ni jukumu la raia kuwasiliana na usimamizi wa uchaguzi ili kuhakikisha kwamba wanasajiliwa. Tofauti ni kwamba usajili wa kujitolea kwqa hiari yako mwenyewe unaweza kuanzishwa na mpigakura mwenyewe (hivyo basi ukawa wa kujianzishia) au halmashauri ya kusimamia uchaguzi (hivyo ukawa umeanzishwa na serikali). Mfumo wa kujianzishia wa usajili wa wapigakura unaweza kuchukuliwa kama kitu cha haja badala ya kikanuni.
Wakati mwingine kuna vizuizi muhumu vinavyoweza kutatiza usajili wa kuanzishiwa na serikali. Kwa mfano, huduma ya posta inaweza kushindwa kuwafikia wapigakura wote au wengi vilivyo. Gharama kubwa zinaweza kuzuia hesabu ya kutoka nyumba hadi nyingine.
Mifumo ya usajili ya kujianzishia wenyewe inaweza kuchukua maumbo mbalimbali:
- Halmashauri ya kusimamia inaweza kubuni vituo vya usajili wa wapigakura, na watu wanaotaka kupiga kura wanalazimika kwenda huko kuwasiliana na maafisa wa uchaguzi. Vituo vinaweza kuwa visivyohamishwa, vya kuhamishwa au vyote viwili.
- Raia wanaweza kujisajili na mashirika mengine kama vile mashirika ya kusajili magari ambayo hubadilishana taarifa zao mara kwa mara na halmashauri ya kusimamia uchaguzi.
- Vivyo hivyo, raia wanaweza kuarifu huduma ya posta kuhusu mabadiliko ya anwani na taarifa hiyo hupelekewa halmashauri ya kusimamia uchaguzi. Katika kisa kimoja, halmashauri ya kusimamia uchaguzi huendeshwa kama idara ya katika huduma ya posta ikiwa na majukumu yaliyofungamanishwa.
- Halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kutunza tovuti ambamo mtu anayetaka kupiga kura anaweza kuchukua fomu za usajili, za kujazwa na kutumwa kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi. Tovuti hiyo inaweza kusaidia usajili wa mtandaoni wa wapigakura.
Kukiwa na mfumo wa kujianzishia usajili, viwango vya usajili huonekana kuwa chini kuliko pakiwa na mfumo ambamo serikali inaanzisha mawasiliano. Hivi ni kwa sababu kwa kiwango kikubwa usajili huo unakuwa wa hiari ya mtu. Hata hivyo, kuna njia za kuimarisha usajili:
- Kuweka vituo vingi vya usajili.
- Kutumia vituo vya kuhamishwa ili kwamba wapigakura wasitembee miendo mirefu kusajiliwa.
- Kamilisha hatua zote za mchakato huo – ikiwemi kupeana kadi za vitambulisho vya wapigakura ikiwezekana – katika hatua moja ya usajili. Hii ni changamoto ya kutiliwa maanani, hasa ikiwa kwamba ni lazima kadi changamano ya kumtambulisha mpigakura itolewe au ikiwa ni lazima rekodi zikaguliwe kuthibitisha utambulisho wa mtu anayejisajili.
- Waruhusu watu kuwasajili watu wa familia zao, hivi kupunguza idadi ya watu ambao ingekuwa lazima kwao kufika kwenye kituo cha usajili wenyewe.
- Teua manaibu wa usajili katika kila eneo ili kuondoa vikwazo vya kiusimamizi.
- Ruhusu usajili kwa njia ya barua ikiwa masharti yamezingatiwa.
- Weka nyenzo zinazoweza kuchukuliwa kwenye kutoka kwenye tovuti ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi.
- Ikiwezekana na ikifaa wezesha raia kujisajili kwenye wavuti.
- Angazia uwezekano wa kuweka rejista ya mpito ya vijana watakaofikisha umri wa kupiga kura katika mwaka mmoja au miwili hivi. Ikiwezekana, wazia kuhimiza usajili kwa kuweka mipango ya elimu kwa wapigakura katika shule za upili.
Usajili unaoanzishwa na Serikali
Usajili unaoanzishwa na serikali hutokana na mtazamo kwamba wasimamizi wa uchaguzi wana jukumu la kujaribu kusajili wapigakura wote. Wanaweza kutimiza jukumu lao kwa njia ya hesabu ya kutoka nyumba hadi nyingine ili kujenga orodha ya muda, au kutunza orodha endelevu au sajili endelevu ya raia iliyo kamilifu na ya kisasa.
Usajili ulioanzishwa na serikali utagharimu zaidi ya usajili wa kujianzishia mwenyewe kwa sababu serikali inapaswa kufanya juhudi ya kuwasiliana na raia wote. Ili mfumo uwe pana na shirikishi, serikali inapaswa pia kuwafikia wapigakura ambao ni wagumu kuwafikia, wakiwemo wale ambao huhama mara kwa mara, wale walio katika maboma yao asilia na wale wasiojibu maombi ya mwanzo ya taarifa kuwahusu. Ingawa ni ghali sana, mfumo wa kuanzishiwa na seriakali utatoa orodha kamilifu ya wapigakura kuliko mfumo wa usajili wa hiari.
Kwa kiwango fulani usajili ulioanzishwa na serikali huwa na nafasi kubwa ya wasimamizi kuwafikia raia wote. Uwezo huu unaweza kuendelea kuwepo katika nchi iliyopimarika kiuchumi kwa sababu mbili:
- Raia wake wana makao ya kudumu yanayohudumiwa na huduma ya kitaifa ya posta.
- Muundo wake wa kusimamia uchaguzi mara nyingi huwa umeimarika na kufadhiliwa vizuri. Ili kusaidia usajili wa wapigakura ulioanzishwa na serikali, halmashauri ya kusimamia uchaguzi hutafuta mikakati ya kutumia deta kwa ushirikiano na mashirika mengine ya serikali ambayo hukusanya taarifa kuhusu raia. Haya yanaweza kuwa pamoja na huduma ya posta, mamlaka ya usimamizi wa makao, ofisi ya kukusanya ushuru, mashirika ya kusajili magari au leseni za madereva, na halmashauri za kusimamia uchaguzi katika viwango vingine vya serikali.
Mkakati Mseto
Kuna kibadala cha tatu, ambamo raia na serikali hushirikaina katika jukumu la usajili. Serikali inapaswa kuchukua hatua za kurahisisha usajili, na wananchi wanapaswa kucheza nafasi yao ya kukamilisha mchakato huo.
Mkakati huu mseto hutumiwa kwa mataifa yasiyostawika kiuchumi ambayo yanaazmia kuongeza viwango vya usajili japo hayana raslimali za kutosha na muundomsingi mwafaka. Katika mkakati huu, serikali huweka tarehe maalumu za usajili uliotangazwa na kuweka idadi kubwa ya vituo vya usajili vikiwemo vile vya kuhamishwa. Raia bado wanalazimika kuchukua hatua ya kwenda katika vituo vyao na kujisajili. Lakini ikiwa usimamizi wa usajili utaamua kutumia mwelekeo wa kuoangaza mbele na ambao ni shirikishi, unaweza kupunguza wakati utakaotumiwa na raia katika kujisajili na kuufanya mfumo huo kuwa rahisi wa kuelewa.
Kwa kweli, hata katika nchi zilizostawika kiuchumi, mifumo ya usajili wa wapigakura mara nyingi hufuata mkakati huu mseto, huku halmashauri ya kusimamia uchaguzi ikianzisha mawasiliano na wananchi wakiwa na jukumu jingine la kuhakikisha taarifa zao za usajili wa wapigakura ni linganifu na za kisasa. Kwa mfano, katika nchi inayotumia orodha endelevu, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kufanya usajili wa kutoka nyumba hadi nyingine katika maeneo yaliyo na viwango vya juu kuhama kama sehemu ya hatua usajili unaolenga makundi maalumu. Ikiwa hakuna yeyote nyumbani wakati wasajili wanapotembelea makao yao, wanaweza kumwachia mkazi huyo kadi ili aijaze na kuirudisha kwa halmashuri ya kusimamia uchaguzi. kwa wakati huo huo, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kuhakikisha uwepo wa fomu za usajili, pengine katika ofisi za posta au kwenye tovuti yake; yeyote anayetaka kupiga kura anaweza kuijaza fomu hiyo na kuirudisha. Raia na serikali wote hivyo basi huchukua jukumu fulani katika usajili wa wapigakura.