Katika kujenga sajili ya raia, hatua ya kwanza ni kutathmini ubora wa taarifa iliyopo kutoka kwa vitovu vingine. Katika visa vingine, vitovu vilivyopo vya kutoa deta vinaafiki kabisa na juhudi hasa hulenga kuhamisha deta inayofaa hadi kwa halmashauri ya kusimamia ucahguzi.
Wajibu wa Serikali ya Mitaa
Serikali za mitaa au kimaeneo mara nyingi huwajibikia utunzaji wa sajili ya raia, kuanzia kwa usajili watoto wanaozaliwa. Ikiwa hata taarifa ya kimsingi kama hiyo haipo, serikali inalazimika kupanga mikakati ya kukusanya deta ya kutumiwa katika sajili ya raia. Hii inafanana na shughuli ya usajili kwa lengo la kutayarisha orodha endelevu ya mwanzo ya wapigakura au orodha ya muda ya wapigakura.
Kinyume na orodha ya muda, kwenye sajili ya raia na orodha endelevu taarifa iliyokusanywa mwanzoni huwa msingi wa kutengeneza orodha hiyo (ilivyotajwa mapema), na kazi inayofuata huchunguza ulinganifu wa deta hiyo na kuisasaisha mara kwa mara. Tofauti na ilivyo kwa sajili ya raia, orodha endelevu hulenga deta ya uchaguzi pekee na hutumiwa kwa manufaa ya uchaguzi pekee. Sajili ya raia yenyewe inaweza kutumiwa kwa shughuli mbalimbali, kama vile kutunza deta ya kimsingi kuhusu jumla ya idadi ya watu, kuchunguza hatua na athari ya huduma za usaidizi kutoka kwa serikali, kuweka rekodi za ushuru, na kuwatambua watu wanaoazmia kuingizwa katika jeshi. Deta hiyo hiyo ya kismingi iliyokusanywa kwa manufaa haya inaweza kutumiwa kwa manufaa ya uchaguzi.
Orodha ya Usajili ni Muhimu katika Kushiriki katika Maisha ya Raia
Wakati wowote ule, sajili ya raia inaweza kutoa orodha ya wapigakura iliyo na taarifa sahihi ili itumiwe katika uchaguzi. Kuorodheshwa mara nyingi huwa lazima katika sajili ya raia, japo huwa kwa kujitolea katika orodha endelevu ya wapigakura au orodha ya muda ya wapigakura. Kwa kuwa sajili ina matumizi mengi, mtu asiye kwenye orodha sajili hiyo hawezi kupiga kura na pia hutengwa vilivyo kutoka kwenye mambo mengi yanayohusu raia. Kulingana na Dkt. Felipe Gonzalez Roura wa Mahakama ya Kitaifa ya Uchaguzi, Argentina, kutojumuishwa katika sajili ya raia ni hali kubwa ya kupoteza haki:
Kando na uhamasishaji wa raia kwa kutimiza haki yao ya kupiga kura na kukamilisha jukumu la huduma ya jeshi, yeyote anayekiuka wajibu huu hana stakabadhi ya kisasa ya kumtambulisha na hivyo ni kama raia aliyekufa. Mtu kama huyo hawezi kufanya kazi kisheria, kupiga kura, au kufanya shughuli yoyote ile. Hawezi kutoka katika nchi hiyo, kujisajili katika asasi zozote za masomo, kshiriki faida za kijamii miongoni na mengine. [1]
Kwa hivyo, katika upeo na wajibu wake mkuu katika maisha ya umma, sajili ya raia ina umuhimu zaidi ya ule wa orodha ya wapigakura. Kule Uswidi kwa mfano, kila mkazi anapaswa kuorodheshwa katika rejista ya watu, ambayo hutoa deta ya kutumiwa kutayarisha orodha ya wapigakura. Jina la yeyote anayepaswa kupiga kura huonekana katika orodha ya wapigakura hata kama mtu huyo anapendelea kutoorodheshwa.
Jukumu la Kihadhi dhidi ya lile la Kibinafsi
Kupangia sajili ya raia kunapaswa kuzingatia wajibu wake mkuu katika maisha ya umma. Kwa kuwa mara nyingi huwa lazima kwa wananchi kuorodheshwa, serikali inapaswa kuwa msitari wa mbele katika kusaidia maendelezo na utunzaji wa sajili hiyo. Ili kufanya hivi, serilakali haina budi kuwa na muundomsingi wa uendeshaji unaoweza kukusanya deta ya muhimu na kutunza sajili hiyo. Mitambo ya hali ya juu ya tarakilishi si lazima: katika nchi nyingine zilizo na mamilioni kumi ya watu, serikali imefaulu kutunza sajili ya raia kwa kutumia kadi za faili. Hata hivyo, matumizi ya tarakilishi hurahisisha kabisa kazi kutunza deta hizo zilizojumuishwa katika sajili ya raia.
Huku serikali ikiwa mstari wa mbele katika kutunza sajili ya raia, wananchi bado mara nyingi wanawajibika kuiarifu serikali hiyo kuhusu mabadiliko katika taarifa zao za kibinafsi. Nchi nyingi hulazimisha utoaji wa ripoti za kuzaliwa au mabadiliko ya makazi katika kipindi fulani cha wakati (hasa kifupi) kwa halmashauri inayoshughulika na kutunza sajili ya raia. Hii ni njia nyingine ambapo sajili ya raia inatofautiana na aina nyingine za usajili wa wapigakura.
Isitoshe, usajili wa kutumiwa kutengeneza orodha ya muda au endelevu unaweza kufaa tu kwa muda fulani. Kwa orodha ya muda, wapigakura wote stahifu wanapaswa kujisajili kwa kila uchaguzi, wawe walipiga kura katika matukio ya chaguzi za awali au la. Hata na orodha endelevu, nchi nyingi hutaka wapigakura waliojisajili kubadilisha kadi zao za utambulisho wa wapigakura au kujisajili upya baada ya muda fulani. Kwa sajili ya raia, hata hivyo, usajili wa mwananchi kupiga kura hauishi bila sababu mwafaka.
Nambari ya Utambulisho wa Raia
Iwe inachukuliwa kama orodha moja inayotumiwa kwa kazi nyingi au kama viziodeta vingi vinavyotumiwa kwa majukumu mengi, sajili ya raia ina sifa moja kuu: hutegemea ugawanaji taarifa katika mashirika au idara zote za serikali, au hufanya kazi katika mipaka ya shirika moja. Ili kurahisisha ugawanaji huo, chombo kinahitajika kianchoweza kutumika kama kiungo kati ya viziodeta au vitengo vya kiusimamizi. Chombo hiki ni nambari ya utambulisho wa raia.
Mifumo takribani yote inayotumia sajili ya raia humpa kila mwananchi, nambari ya kudumu, ama pale kuzaliwa kunaposajiliwa au anaposajiliwa kama mtu mzima (hasa kati ya umri wa miaka 16 na 21). Nambari hiyo ni gundi inayounganisha viziodeta mbalimbali vinavyotoa taarifa kwa sajili. Rekidi za kipekee za utambulisho zinaweza kuhifadhiwa pahali pamoja, na zote ziunganishwe kwa kutumia nambari hiyo ya utambulisho. Hili huondoa haja ya kutoa kadi za utambulisho wa wapigakura kwa raia katika siku za kukaribia uchaguzi, hivyo basi kumudu kupunguza gharama ambayo ingetumika.
Halmashauri ya Kusimamia Uchaguzi katika Mfumo wa Sajili ya Raia
Katika mfumo unaotumia sajili ya raia, kuna vibadala vingi vya jinsi halamshauri ya kusimamia uchaguzi inavyopaswa kujiendesha. Ikiwa mtindo wa demokrasia umeingizwa vilivyo, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kuwa katika wizara ya serikali, kama vile ofisi ya kushughulikia ushuru – ingawa kwa kawaida kama kitengo huru cha usimamizi. Ikiwa demokrasia haijakita mizizi ya kutosha, haitakuwa vizuri kulipa tawi la utendaji la serikali udhibiti dhidi ya usimamizi wa uchaguzi. Suala kuu ni pale ambapo halmashauri ya kusimamia uchaguzi inapaswa kuwekwa ili iweze kutoa ukaguzi wa kibinafsi kuhusu ufaafu wa deta iliyotumiwa kwa usajili wa wapigakura. Jibu litatofautiana kutoka muktadha mmoja hadi mwingine.
MAREJELEO
[1] Dkt. Felipe Gonzalez Roura, “Rejista ya Uchaguzi ya Argentina,” katika Rejista za Uchaguzi, karatasi iliyowasilishwa kwa Kongamano la Pili la Muungano wa Asasi za Kusimamia za Amerika ya Kati na Karibia, Santo Domingo, Jamhuri ya Dominika, Novemba 23–26, 1987.