Punde orodha ya kwanza ya wapigakura ikishatolewa, makundi husika yanapaswa kuruhusiwa kuidurusu orodha hiyo. Uwepo wa orodha hiyo ni muhimu katika kukuza imani katika uchaguzi huo. Ili kuwezesha umma kuipata orodha hiyo, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inapaswa kutumia njia kabambe za mawasiliano. Uchapishaji wa orodha hiyo ya kwanza unaweza pia kutoa nafasi nzuri kwa elimu kwa wapigakura.
Mikakati ya kutumia vyombo vya habari
Mbinu mbalimbali za mawasiliano zinaweza kutumiwa katika kueneza orodha hiyo. Moja ni kampeni za televisheni na redio; mabango; matangazo ya magazetini, karatasi za mikononi na posta vinaweza kupiga jeki mbinu hii au vyenyewe kuwa njia kuu ya kueneza kampeni hiyo ambapo vyombo vya kielektroniki vya habari havipo. Kampeni hiyo huwaarifu wapigakura kwamba orodha ya kwanza ipo na kuwaarifu pale wanapoweza kwenda kuikagua – pengine kwenye ofisi ya usajili au kituo kingine. Kunaweza kuwa na mipaka kuhusu taarifa ambayo wapigakura wataruhusiwa kuona. Ili kulinda usiri kwa mfano, wapigakura wanaweza kuruhusiwa kukagua taarifa zao pekee na si orodha nzima.
Kueneza orodha hiyo kunaweza kuwa ghali, hasa ikihusisha matangazo makubwa ya kibiashara. Kibadala kingine cha kuwaarifu wapigakura kwamba wanaweza kukagua orodha hiyo ni matumizi matangazo ya huduma za umma. Hizi mara nyingi huwa nafuu kuliko matangazo ya kawaida japo huenda yakakosa umaarufu wa kutosha. Ujumbe wa kimsingi utakaowasilishwa ni, “Umesajiliwa kama yafuatayo ni ya kweli…” Wapigakura hawahitajiki siku zote kuthibitishwa uwepo wao kwenye orodha. Mpigakura anaweza kupewa risiti baada ya kujisajili, au kutumiwa kadi ya kuthibitisha kusajiliwa kwake na kuonesha wakati na mahali atakakopigia kura.
Hali mbalimbali hutaka mikakati mbalimbali ya uenezi. Katika nchi zilizo na historia ndefu ya kufanya chaguzi huru na za haki na kutumia uongozi wa kidemokrasia, mkakati huo unaweza kujikita kwa matangazo ya huduma za umma pamoja na kadi yenye taarifa iliyotumwa kwa njia ya barua kwa wapigakura wote waliosajiliwa. Katika nchi ambamo chaguzi na demokrasia ni uvumbuzi wa hivyo karibuni, mkakati huo unaweza kuwa na bejeti kubwa na kuunganishwa na juhudi za elimu kwa wapigakura.
Mikakati isiyotumia vyombo vya habari
Kando na mikakati inayotumia vyombo vya habari kwa mapana, kuna njia nyingine za kudokeza uwepo wa orodha ya kwanza. Moja ni kubandika tangazo kuhusu orodha hiyo kwenye jingo linaloingiwa na umma au eneo lolote la umma. Katika jamii nyingine, tangazo hilo linaweza kutolewa kwa kutumia ngoma au kupitia kwa maigizo ya kithieta. Isitoshe, nakala za orodha hiyo kwa kawaida hutumwa moja kwa moja kwa vyama vya kisiasa (inavyohitajika kisheria) au makundi mengine husika. Kwa ufupi, kuna njia nyingi za kueneza habari kuhusu orodha hiyo. Changamoto, zikiwepo, zitakuwa za kifedha.
Kulinda orodha hiyo
Orodha ya wapigakura kwa kawaida inapaswa kutumiwa kwa shughuli za uchaguzi pekee, hivyo hakuna mkakati wowote wa uenezaji unaopaswa kukiuka kanuni hii. Shida ya kuionysha orodha hiyo katika sehemu za umma ni kwamba inaweza kuraruliwa au kuchafuliwa. Badala yake, maeneo mengi ya kiusimamizi huwa na vituo vya masahihisho ya orodha, vilivyo na wafanyakazi watakaokagua jina la mtu akiomba kufanyiwa hivyo. Changamoto iliyopo ni kuthibitisha usajili huo bila kuwatatiza wapigakura na bila kutumia raslimali nyingi zilizopo kwa shughuli hii.