Kufikia siku ya uchaguzi, nakala ya orodha ya mwisho ya wapigakura ya kutumiwa katika maeneo pana ya uchaguzi inapaswa kuwepo kwenye vituo vya kupigia kura. Hii ni ya lazima, na mipango inapaswa kuhakikisha kwamba mahitaji hayo yanaafikiwa. Jinsi itakavyoafikiwa huenda ikatofautiana. Katika nchi nyingine, ofisi za kusimamia uchaguzi zinawajibikia kutayarisha orodha ya kwanza, kunakili mabadiliko, na kukamilisha na kuchapisha orodha ya mwisho. Wajibu huo hivyo basi kwa kiwango kikubwa umegatuliwa, ingawa viwango vinavyofanana hutumiwa katika nchi nzima, na orodha ya mwisho vinapaswa kusambazwa kwa kuwa imetengezwa katika eneo la matumizi yake. Nchi nyingine huchukua mwelekeo wa kutoa orodha katika kituo kimoja kikuu, hivyo basi kuweka haja ya kutumiwa kwa mbinu mbalimbali za kusambaza orodha hizo kwa ofisi za kieneo. Kwa kiwango kikubwa orodha hizi husambazwa kwa kutumia vyombo vya kielektroniki vya kuhamisha deta, kwa kutumia ama njia zilizounganishwa kwa kutumia nyaya, au mawasiliano yasiyounganishwa kwa nyaya au setilaiti. Hata hivyo, nchi nyingine bado zinachapisha orodha katika vituo vikuu na kusambaza nakala hizo zilizochapishwa hadi kwa ofisi za maeneo ya matumizi yake. Kwa mbinu yoyote ile inayotumika, usalama wa usambazaji ni muhimu katika kudumisha kuaminika kwa mfumo wa usajili wa wapigakura.
Kutumiwa kwa Orodha ya Wapigakura na Vyama na Wagombea
Kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi, orodha ya wapigakura hutoa maelezo kuhusu ustahifu wa kupiga kura kwa kila mtu aliyeorodheshwa. Kwa vyama vya kisiasa na wagombea, orodha hiyo hutoa majina na taarifa kuhusu jinsi ya kuwasiliana (hasa anwani zao) kuhusu watu wote wanaostahili kupiga kura katika uchaguzi unaokaribia. Vyama vya kisiasa na wagombea mara nyingi hufanya shughuli za kupita hapa na pale, hivyo basi kuwasiliana na wapigakura na kutambua wale watakaowaunga mkono na kusambaza ujumbe wa kampeni.
Shughuli hizi za kupita hapa na pale pia huvipa vyama na wagombea fursa ya kutafuta usaidizi wa watu wa kujitolea na usaidizi wa kifedha katika kampeni zao za uchaguzi. Hii ni sababu moja ya kupata anwani za barua za wapigakura wakati wa usajili wa wapigakura. Mara kwa mara, anwani za makazi ni sawa na anwani ya barua lakini hili haliwi hivyo kila mara hasa katika maeneo ya mashambani. Hao wanaotembeatembea kutoka eneo moja hadi jingine wakati mwingine huwauliza wapigakura kama wanaweza kukubali ishara za kampeni zinaweza kuwekwa kwenye maboma yao au karibu na maboma yao, au kutembelea majirani na marafiki wao kwa niaba ya wagombea au chama.
Vyama na wagombea hutumia mitindo ya kutambua uwezekano kwamba mpigakura atawaunga mkono katika uchaguzi huo. Wapigakura wanaweza kutambuliwa kama wanaoweza kuwa wafuasi, wafwasi watarajiwa au wasioweza kuwa wafuasi, na hivyo mkakati wa kampeni za mgombea utatofautiana kwa kila kundi. Wafuasi waliojitolea, kwa mfano, mara nyingi hupokea taarifa ya kupiga jeki shughuli zao. Mwelekeo hima unaweza unaweza kutumiwa kwa wafwasi watarajiwa, ikiwemo ziara ya kibinafsi kutoka kwa mgombea huyo ikiwezekana. Wapigakura kura walio na uwezekano mdogo sana wa kumuunga mkono mgombea huyo wanaweza kupuuzwa, kwa matumaini kwamba mawasiliano ya kiwango cha chini yatawafanya kukosa ari ya kushiriki katika uchaguzi na pengine kushiriki. Vyama na wagombwa pia huto usaidizi, ikiwemo kuwasafirisha watu hadi kwenye vituo vya kupigia kura, kwa wapigakura ambao wametambuliwa kama walio na uwezo wa kuwa wafuasi.
Mchango wa Vyama na Wagombea kwenye Orodha ya Wapigakura
Kampeni katika nchi nyingi za kidemokrasia huwa na mifumo yote miwili, sifa kuu au zilizogatuliwa, na zinaweza kuwa na athari ya kitaifa na vilevile ya kieneo. Kampeni za kitaifa zinaweza kutekelezwa kupitia kwa vyombo vikuu vya habari, kama vile redio, televisheni na magazeti; havitumii orodha za wapigakura. Kwa kampeni za kieneo hata hivyo, kipengele kikuu mara nyingi huwa kutembea kutoka nyumba moja hadi nyingine na orodha ya wapigakura huwa kifaa muhimu. Kwa sababu hiyo, vyama na wagombea wanaweza kushughulika na mara nyingi kukaribisha wachangizi kwenye mchakato wa kutengeneza orodha ya mwisho ya wapigakura.
Wajibu wa vyama katika uchunguzi na usahihishaji wa orodha unapaswa kuchukuliwa kwa hadhari na halmashauri ya kusimamia uchaguzi. Kwa kutumia taarifa ambazo vyama vinaweza kutoa, wasimamizi wa uchaguzi wanapaswa kutahadhari dhidi ya kutegemea watu walio na nia za kupendelea pande mbalimbali.
Wakati wa kutoa orodha ya wapigakura ni kipengele muhimu kwa vyama vingi vya kisiasa. Vyama na wagombea hupokea orodha ya kwanza ya wapigakura mapema katika kampeni, na kuitumia kwa manufaa ya kampeni. Orodha ya mwisho ya wapigakura inaweza kuchapishwa baadaye ili vyama viweze kuitumia vilivyo. Hata hivyo, huviwezesha kuangalia iwapo mabadiliko waliyoomba kwenye orodha ya kwanza yamefanywa. Aidha, hutoa nafasi kwa vyama kuidhinisha rasmi ubora wa orodha hiyo.