Lengo la shughuli ya usajili wa wapigakura ni kujenga orodha pana ya wapigakura itakayokuwa ya kisasa na linganifu iwezekanavyo kwenye siku ya uchaguzi. Uamuzi kuhusu wakati wa kufunga usajili hutegemea hali maalumu katika kila eneo au hali. Miongoni mwa vipengele vingine, uamuzi huo unaweza kuathiriwa na mahitaji ya uteuzi wa mgombea. Wagombea wanapaswa kila mara kuwa na karatasi za uteuzi wao zilizotiwa saini na wapigakura wastahifu, wakati mwingine mamia yao. Ili kuthibitisha kwamba wanaotia sahihi hizo ni wapigakura wastahifu, angaa orodha ya kwanza ya usajili wa wapigakura inapaswa kuwepo.
Vifuatavyo ni vipengele vingine vinavyoathiri uteuzi wa siku ya kufunga usajili:
- Muda unaotumika kutoa orodha ya mwisho ya wapigakura, uliokadiriwa kwa misingi ya dharura ya kusajiliwa kabla ya uchaguzi.
- Iwe kwamba kushiriki katika uchaguzi ni lazima au wa kujitolea. Katika mifumo ambamo usajili ni wa lazima, tarehe ya kufunga inaweza kuwa mapema kwa sababu wapigakura wanajua kwamba wanaweza kutozwa faini wakikosa kuhakikisha kwamba taarifa za usajili wao ni za kisasa.
- Kiwango cha kushughulikiwa kwa pamoja kwa orodha ya wapigakura. Mifumo iliyo na viwango vikubwa vya ugatuzi inaweza kuwa na uwezo wa kukabili mabadiliko katika taarifa za usajili haraka, hivyo kuuwezesha kuufunga usajili huo baadaye.
Fanya Kazi kinuyuma ili kutambua Tarehe ya Kufunga shughuli hiyo
Ili kuweka tarehe ya mwisho ya usajili, ni bora kuanza na tarehe ya uchaguzi na kufanya kazi kinyuma, huku ukizingatia vipengele vingine muhimu vya shughuli ya uchaguzi. kwa mfano:
- Ni muda kiasi gani unaohitajika kutoka kwa wakati ambao koti ya masahihisho hadi wakati wa utoaji na usambazaji wa orodha ya mwisho ya wapigakura?
- Je, koti ya masahihish itakaa kwa siku, wiki, wiki mbili au muda zaidi?
- Je, ni muda kiasi gani utakaohitajika kutoka kwenye kukamilika kwa orodha ya kwanza ya wapigakura hadi koti itakapoanza vikao vyake?
- Ni muda kiasi gani unaohitajika kusahihisha orodha ya mwanzo ya wapigakura?
- Ni muda kiasi gani kabla ya siku ya uchaguzi ambapo vyama au wagombea watapata orodha za mwanzo za wapigakura? Je, inapaswa kuwa wiki moja, mwezi mmoja, miezi mitatu au muda fulani kabla ya uchaguzi?
- Je, itachukua muda kiasi gani kusajili wapigakura wote na kutoa orodha ya mwanzo ya wapigakura? Kila kigezo kinaweza kuwa na athari kwenye jumla ya wakati unaohitajika kwa shughuli ya usajili.
Kuwa na Uhalisia
Bila shaka, jukumu la usajili ni kutoa orodha ya mwisho ya wapigakura. Katika mfumo unaotumia orodha ya muda, hatari ya kufeli huwa kubwa kwa sababu sehemu kubwa ya kazi hiyo ni lazima ikamilike katika muda mfupi, hasa punde kabla ya uchaguzi. Hili bila shaka huongeza shinikizo la kufaulu, hasa kadiri tarehe ya uchaguzi inavyokaribia.
Wasimamizi wa uchaguzi kiasilia hupendelea kutoa orodha ya wapigakura yenye usasa, ulinganifu na ukamilifu iwezekanavyo, japo wanapaswa kuwa na uhalisia kuhusu changamoto za uendeshaji zinazohusiana na uwezo wa kiusimamizi wa halmashauri ya kusimamia uchaguzi katika viwango vya kitaifa na kieneo. Ili kuweza kukabili changamoto hizo, wasimamizi wanapaswa kuwa na fedha za kutosha, nyenzo na raslimali za wafanyakazi. Wakati mwingine kufaulu kwa shughuli hiyo kutategemea uwepo wa muundomsingi thabiti wa kijamii au kiserikali unaoweza kukabiliana na mahitaji haya. Ikiwa wapangaji wamekosa kukadiria vilivyo wakati unaohitajika katika kutoa orodha ya wapigakura, ni bora kuchukua mwelekeo wa upole na wa kusamehe badala ya kuwa thabiti na unaohitaji shughuli nyingi.
Tarehe za mwisho na Sajili ya Raia
Kwa orodha ya muda na endelevu ya wapigakura, mara nyingi kuna tarehe ya mwisho ya kufunga usajili kwa matumizi katika orodha ya mwanzo ya wapigakura na orodha ya mwisho ya wapigakura. Kinyume cha haya, usajili haufungwi katika kutengeneza sajili ya raia kwa sababu ni muhimu kabisa katika utekelezaji huduma za serikali.
Hata hivyo kunaweza kuwa na tarehe ya mwisho ya kufunga ubadilishaji wa taarifa kwenye sajili ta raia ili itumike kabla ya uchaguzi. Kwa mfano, mtu akitoa taarifa kuhusu mabadiliko ya makazi baada ya kukamilika kwa makataa, mtu huyo anaweza kuruhusiwa haki ya kupiga kura tu katika eneo pana la uchaguzi ambako aliishi kabla ya kuhama. Watu ambao hawatakuwa wameorodheshwa katika sajili kabla ya siku ya kufunga usajili huenda wasiruhusiwe kupiga kura. Katika hali halisi, hili huwa halifanyiki mara kwa mara kwa sababu usajili huo mara nyingi huwa wa lazima ili kutumiwa kwa sajili za raia.