Upigaji kura wa mapema ni sifa ya kawaida katika mifumo ya chaguzi za kidemokrasia. Huruhusu upigaji kura kwa watu ambao wanastahili kupiga kura lakini hawawezi kufika kwenye vituo vya kupigia kura kwenye siku ya uchaguzi. Kuna hali mbili zinazohusisha usajili na upigaji kura wa mapema:
- Mtu ambaye hajasajiliwa anataka kupiga kura katika kituo cha upigaji kura cha mapema. Uamuzi unapaswa kufanywa iwapo mtu huyo anaweza kujisajili na kupiga kura. Huu si uamuzi wa kiusimamizi, bali mmoja tu unaofanywa na wanasiasa na kufafanuliwa katika sheria kuhusu uchaguzi. Kanuni hiyo inaweza kutarajiwa kutumiwa pia katika hali hii na katika kisa cha mtu ambaye hakusajiliwa na anataka kupiga kura katika vituo vya kawaida vya upigaji kura kwenye siku ya uchaguzi. Sheria hiyo inaweza kumpa msimamizi wa uchaguzi katika kituo cha mapema cha kupigia kura mamlaka ya kuongeza mtu huyo kwenye orodha ya wapigakura. Sheria inaweza pia kufafanua umbo la kura na, ikiwezekana bahasha ya kura itakayotumika.
- Upigaji kura wa mapema umefanyika na orodha ya wapigakura inapaswa kusasaishwa ili itumiwe kwenye kituo cha kupigia kura siku ya uchaguzi. Utaratibu mwafaka wa kusasaisha unahusisha kudondoa majina ya wale waliopiga kura kwenye vituo vya mapema vya uchaguzi. Hili huhakikisha kwamba yeyote aliyepiga kura katika kituo cha mapema hapigi kura tena katika vituo vya kawaida siku ya uchaguzi.